Posts

Showing posts from June, 2026

WADAU ZAIDI YA 200 SEKTA YA AFYA KUSHIRIKI MKUTANO WA KIMATAIFA WA SNOSSA 2026 DAR

Image
  Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline      DAR ES SALAAM  TAASISI ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Kimataifa wa Society for Neuro-Oncology Sub-Saharan Africa (SNOSSA) 2026, utakaofanyika ijini Dar es Salaam. Mkutano huo  ukitarajiwa kukutanisha wataalamu, watafiti na wadau wa sekta ya afya zaidi ya 200 kutoka ndani na nje ya Afrika kujadili maendeleo ya tiba ya magonjwa ya mfumo wa fahamu, hususan saratani za ubongo na mfumo wa fahamu. Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Mhe. Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya, amesema mkutano huo utatoa fursa ya kujadili mbinu za kisasa za kugundua mapema magonjwa ya mfumo wa fahamu, matumizi ya teknolojia za kisasa katika uchunguzi wa radiolojia, pamoja na matibabu sahihi na ya wakati. Aidha, washiriki watajadili namna ya kuboresha upatikanaji wa huduma za afya, kuimarisha ushirikiano wa kitaaluma na kuendeleza tafiti zinazolenga kuboresha huduma kwa wagonjwa. Dkt. Mpoki ameongeza kuwa kupitia mkutano ...

WAZIRI ULEGA :HAKUNA SABABU YA KURUHUSU WATU WACHACHE KUVURUGA AMAN NA UTULIVU WA NCHI YETU.

Image
 Na Mwandishi wetu,DmNewsonline                    ARUSHA  WAZIRI wa Ujenzi, Abdallah Ulega, amewataka Watanzania kuendelea kuilinda amani na utulivu wa nchi, akisisitiza kuwa hakuna sababu ya kuruhusu watu wachache kuitumia hali hiyo kwa maslahi yao binafsi au ya wengine. Akizungumza jijini Arusha wakati wa ukaguzi wa miradi ya miundombinu, Ulega amesema kuna baadhi ya watu wanaotamani kuona Tanzania ikiingia katika vurugu ili wapate hoja za kuwasilisha kwa wanaowaunga mkono, lakini akasisitiza kuwa hilo halitafanikiwa. "Kuna watu wanatamani tuwe na vurugu. Tusipokuwa na vurugu wanakosa cha kusema kwa mabwana zao. Amani tuliyonayo tusiikubali itumike vibaya kwa maslahi ya watu wachache," amesema Ulega. Ameeleza kuwa Serikali itaendelea kuhakikisha mazingira ya amani, utulivu na maendeleo yanadumishwa huku ikiendelea kutekeleza miradi ya maendeleo kwa manufaa ya wananchi. Ulega pia ametoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikian...

TAZAMA UTABIRI WA HALI YA HEWA JUNI 29 2026

Image

TESHA AICHANGIA FFC MILIONI 10, ATAKA WANAKWAYA WAJIKOMBOE KIUCHUMI KUPITIA MIRADI

Image
  Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline            DAR ES SALAAM  MWENYEKITI  wa Bodi ya Ofisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA), Victor Tesha, amewataka wanakwaya wa Flying Family Choir (FFC) kuanzisha miradi ya maendeleo itakayokuwa chanzo cha kuongeza kipato na kuwasaidia kujikomboa kutoka katika umaskini. Tesha amesema hayo Juni 28,2026 katika tamasha la kwaya hiyo lijulikanalo FFC Corporate Encore 2026, lililofanyika katika Ukumbi wa Cardinal Rugambwa, Oysterbay, jijini Dar es Salaam, na kuhudhuriwa na watu mbalimbali, akiwemo Askofu wa Jimbo Katoliki la Morogoro, Lazarus Msimbe. FFC Kwaya inaundwa na wanakwaya kutoka madhehebu matatu ya Kikristo ambayo ni Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Kanisa la Anglikana na Kanisa Katoliki, wakishirikiana kupitia huduma ya uimbaji wa injili. Akizungumza katika tamasha hilo, Tesha ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Wadogo wa Madini Tanzania (FEMATA), amesema wana...

VIJANA 10 WAFUZU FAINALI SHINDANO LA VIJANA UCHUMI CHALLENGE 2026

Image
  Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline                     PWANI  VIJANA  wapatao kumi (10) kutoka baadhi ya mikoa mbali mbali   wamefanikiwa kutinga katika kinyang'anyiro cha  shindano la Vijana uchumi Challenge kwa mwaka wa 2026 ambalo kilele chake kinatarajiwa kufanyika Julai 6 mwaka huu katika ukumbi   Mikutano wa Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC), jijini Dar es Salaam. Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Jenifa Omolo  ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa  halfa ya kufunga kambi rasmi ya vijana wapatao 100 ambao walikuwa wameweka kambi ya siku nne katika shule yaa uongozi wa Mwalimu Julias Nyerere iliyopo Kibaha Mkoa wa Pwani. Katibu Oomolo amesema kwamba kambi hiyo ilikuwa na vijana wapatao 100 kutoka mikoa mbali mbali ya Tanzania bara na visiwani ambapo wameweza kufanyiwa usahili na  kufanyiwa mchujo kutoka kwa majaji mahiri wap...

RAIS SAMIA KUFUNGUA MKUTANO WA SABA WA MADINI NOVEMBA 19,2026 DAR

Image
 Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline       DAR ES SALAAM  RAIS   Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufungua rasmi Mkutano wa Saba wa Madini na Uwekezaji Tanzania (TMIC 2026) utakaofanyika Novemba 19 hadi 21, 2026 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam. Akizungumza leo Juni 27, 2026 wakati wa uzinduzi wa TMIC 2026, Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, amesema serikali imeamua kujenga uchumi wa viwanda unaotokana na madini kwa kuwekeza katika uchakataji na uyeyushaji wa madini badala ya kuendelea kuuza malighafi. Amesema kaulimbiu ya mkutano huo, "Madini Yaliyoongezwa Thamani: Chachu ya Ukuaji wa Viwanda na Uchumi," inaakisi dira ya serikali ya kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha uchakataji wa madini barani Afrika. Kwa mujibu wa Mhe. Mavunde, amesema Tanzania tayari ina viwanda vinane vya kusafisha dhahabu, huku Mkoa wa Dodoma ukiwa na viwanda tisa vinavyojengwa na vinavyoendelea na uzalishaji pamoja na kiwanda kikubw...

KING DODO LA BUSH KUWA KUTANISHA WA CONGO JUNI 3 ,KUSHEREKEA UHURU.

Image
  Timothy Marko DmNewsOnline          DAR ES SALAAM.  KATIKA Kuadhimisha miaka(66) siku ya Uhuru wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Congo (DRC) June 3,Mwaka huu , Baadhi ya Wanamuziki wenye Asili ya Nchi hiyo  waishio Nchini Tanzania wamesema kuwa wanatarajia kusherekea siku ya Uhuru wa Nchi hiyo wakiwa Tanzania. Akizungumza Leo juni 26,2026 jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa wanamzikihao waishio Nchini Tanzania King Dodo la Bush amesema katika Maadhimisho hayo yanatarajiwa kuhudhuliwa na Wanamziki wa Congo waliowahi kuishi Nchini Tanzania akiwemo Nyosh Eli sadat kutoka Fm Accademia pamoja Christian Bela. "Tamasha hili linaenda sambamba na Shukrani kwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan amekuwa akitulinda nakutupa Ushirikiano katika Biashara na muziki kwa wa kongo waishio Nchini Tanzania "Amesema King Dodo la Bush. King Dodo Ameongeza kuwa Tamashahilo, la Burudani ya Wanamziki wa Congo waishio Nchini Tanzania ,linatarajiwa kufanyika hotel ya Montana...

TRA YAJITOSA KUSAIDIA JAMII

Image
 Na Eliasa Ally DmNewsonline           IRINGA  MAMLAKA  ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Iringa  imeendelea kuonyesha mshikamano na jamii kwa kuwasaidia wagonjwa wasio na uwezo wa kulipia gharama za matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa. Zoezi hilo limefanyika Juni 25, 2026, ikiwa ni sehemu ya shughuli zinazoendelea kuelekea maadhimisho ya miaka 30 tangu kuanzishwa kwa TRA. Mkurugenzi wa idara ya fedha kutoka TRA Dinah Msuya amesema TRA wamekabidhi misaada mbalimbali ikiwemo malipo ya baadhi ya bili za matibabu kwa wagonjwa wenye uhitaji, pamoja na zawadi kwa wagonjwa na wauguzi wanaotoa huduma hospitalini hapo. Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa, Dkt. Alfred Mwakalebela, ameipongeza TRA kwa hatua hiyo na kutoa wito kwa taasisi nyingine za umma na binafsi kuiga mfano huo kwa kuwasaidia wananchi wenye mahitaji mbalimbali, hususan katika sekta ya afya. Nae mmoja wa wagonjwa walionufaika na msaada...

SERIKALI YASISITIZA ULINZI WA MASLAHI YA WAFANYAKAZI KUPITIA HIFADHI YA JAMII

Image
Na Mwandishi wetu,DmNewsTz Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Ajira na Mahusiano ya Kazi, Deus Sangu, amewataka waajiri nchini kuhakikisha wanawasilisha michango ya hifadhi ya jamii ya wafanyakazi wao kwa wakati ili kulinda maslahi yao na kuwawezesha kunufaika ipasavyo na mafao wanayostahili wanapostaafu. Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa 67 wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Waziri Sangu amesema Serikali inaendelea kusimamia mifuko ya hifadhi ya jamii ili kuhakikisha wafanyakazi wanapata usalama wa kipato baada ya kustaafu, huku akisisitiza umuhimu wa waajiri kutekeleza wajibu wao kwa mujibu wa sheria. “Tunawaomba waajiri wote nchini kuhakikisha wanawasilisha michango ya wafanyakazi kwa wakati. Hii ni haki ya msingi ya mfanyakazi na ndiyo inayomuwezesha kuwa na uhakika wa maisha bora baada ya kustaafu. Serikali itaendelea kusimamia utekelezaji wa wajibu huu kwa manufaa ya wafanyakazi na uchumi wa taifa,” amesema Sangu. Waziri huyo pia amezungumzia malalamik...

CHAUMA YAITAKA SERIKALI KUTENGENEZA MIFUMO WEZESHI KWA VIJANA KUJIKWAMUA KIUCHUMI.

Image
   Timothy Marko DmNewsOnline             DAR ES SALAAM.  CHAMA cha Ukombozi wa umma (CHAUMA) kimeitaka Serikali kuwatengenezea Mazingira mazuri kundi la Vijana  ya kiuchumi ili waweze kujikwamua na kuondokana na tatizo la Ukosefu wa ajira Nchini. Akizungumza juni 24,2026 jijini Dar es Salaam Mratibu wa jukwaa la Vijana wa Chama hicho (JUVICHA)Masoud Mambo amesema Vijana takriban 20,000,000 wanakabiliwa na tatizo la Ukosefu wa Ajira huku 800,000 ndio wapo katika ajira isiyorasmi  "Licha ya kuwepo kwa Mikopo kwa Vijana ,BodaBoda haiwezi kuwa mbadala wa ajira kwa Vijana Amesema Mambo. Mambo Ameongeza kuwa Pamoja na Serikali kutenga takribani Shilingi trioni 62.33 Bado maisha ya Maafisa Usafirishaji (BodaBoda) wanaishi maisha magumu nakwamba Chama hicho kitaendelea kusimamia Ajenda za Wananchi hususa Vijana.  "Katika Mkutano wa kimataifa wa vijana wa Umoja wa Mataifa uliofanyika mwaka 1991 ,ulianisha Changamoto za kiuchumi na...

FILAMU YA KIKULACHO KUONESHWA KUPITIA YOUTUBE KUANZIA SASA.

Image
 Timothy Marko DmNewsonline      DAR ES SALAAM.  MSANII wa Bongofleva Barnaba Elias (Barnaba Class) amesema kuwa uzoefu wake katika soko la Filamu Nchini ulianza kabla ya kuanza mziki wa bongofleva nakusisitiza kuwa tasnia hiyo kwake siyo jambo jipya. Amesema hayo leo Juni 24,2026 jijini Dar es salaam wakati wa kutambulisha seasoni ya 1 ya Kikulacho ambayo imeandaliwa na Kampuni ya Hightable Film nakwamba itakua inaomeshwa kupitia mtandao ya YouTube kwanza sasa. "Nimeamua kuipeleka Filamu hii kwenye YouTube ninaamini kuwa itapata wataamaji wengi ikilinganishwa na kwenye Tv kwasababu baadhi ya Watazamaji hawana visimbuzi vinavyoonesha Filamu,hii inasababisha baadhi ya Watazamaji kukosa uhondo" amesema Barnaba  Nakuongeza kuwa"Filamu hii nimeigiza katika viwango vya hali ya juu ikilinganishwa na Filamu za kutoka Nigeria na Afrika Kusini,hivyo watazamaji watafurahia kutazama Filamu ya Kikulacho". Aidha amesema kuwa amefurahishwa na msanii mwenzake  Gabo Z...

SERIKALI KUTOA ML.50 KWA KINARA SHINDANO LA VIJANA UCHUMI CHALLENGE 2026

Image
   Na Mwandishi wetu,DmNewsonline                 PWANI    SERIKALI  imekuja na mpango kabambe  wa kuanzisha shindano  linalojulikana kwa jina la Vijana uchumi Challenge lenye lengo la kuwakutanisha vijana mbali mbali ili kutoa mawazo  yenye kuleta tija katika kuisaidia Serikali katika nyanja tofauti  ikiwemo uchumi na maendeleo. Hayo yamebainishwa na  Naibu Katibu  Ofisi ya Rais maendeleo ya vijana Dkt.  Kedmon Mapana  wakati wa halfa ya uzinduzi rasmi wa kambi maalumu  kwa ajili ya usahili wa vijana wapatao 100 bora  ambao wamepata fursa ya kuchaguliwa kati ya vijana elfu 7852 walioshiriki hapo awali kutoka mikoa  27 ya Tanzania bara na visiwani. Pia amebainisha kwamba ana imani vijana hao  100 ambao wamechaguliwa na kuweka kambi wataweza kuleta matokeo chanya na kwamba serikali itaendelea kushirikiana nao bega kwa bega na kuchukua mawazo yao ambayo watakwenda k...

JESHI LA POLISI KUENDELEA NA UCHUNGUZI MAUAJI MBEZI.

Image
   Timothy Marko, DmNewsonline        DAR  ES SALAAM.  JESHI la polisi Kanda Maalumu ya Dar es  Salaam limesema linaendelea na Uchunguzi wa kina juu ya Ramadhan Jafarry Muno (47) Baada kudaiwa kupotea huko  Mbezi Wilaya ya Ubungo akiwa kwenye  Nyumba yake.  Akizungumza Leo juni 23,2026 jijini Dar es Salaam Kamishna wa Polisi  Kanda Maalumu ya Dar  es Salaam ( CP) Jumanne Murilo  amesema kuwa tukio hilo lili tokea juni 16,mwaka huu huko Mbezi Kimara Wilayani  Ubungo, Baada ya Jeshi hilo kutarifiwa kuwa mtu huyo amepotea katika Mazingira ya kutatanisha. "Katika Uchunguzi wa awali Jeshi la polisi  tulibaini kuwa aliye fanya tukio hilo ni Mtoto wa Marehemu huyo Juma Ramadhani(21) Ambapo alieleza kuwa Amemuuwa Baba yake" Amesema Kamanda Murillo.  Murilo Ameongeza kuwa Jeshi hilo linaendelea na Uchunguzi wa mtoto huyo kubaini chanzo halisi cha kumua Baba yake. Amesisitiza Baada ya Uchunguzi wa  tuki...

DEOGRATIUS NDEJEMBI KUTOWAVUMILIA WACHELEWESHAJI WA MIRADI VIJIJINI.

Image
  Timothy Marko DmNewsOnline                DAR ES SALAAM WAZIRI wa Nishati Deogratius Ndejembi amesema Serikali Hatowavumilia Wakandarasi Wazawa watakaochelewesha Miradi ya Umeme kwa wakati ,Na baadala yake watanyang'anywa Zabuni hiyo nakutopewa tena katika Miradi hiyo. Akizungumza Leo juni 22,2026 jijini Dar es Salaam  Waziri Ndejembi amesema kuwa Serikali imelenga kuimarisha upatikanaji wa umeme katika maeneo ya vijijini ili kuweza kuchochea Shughuli za  Kiuchumi.  "Umeme ni hitaji muhimu kama ilivyo mahitaji Mengine,Siku hizi Umeme sio anasa bali nikichocheo kizuri cha Kiuchumi "Amesema Waziri Ndejembi.  Ndejembi Ameongeza kuwa Umeme ni Nyenzo Muhimu katika kuimarisha sekta ya Elimu na kukuza Mazingira ya kujifunza kwa Wanafunzi mashuleni,nakukuza Shughuli za kiuchumi.  Amesisitiza kuwa katika Dira ya Maendeleo 2050 Umeme ndio Nyenzo Muhimu katika Utekelezaji wa  Dira ya Maendeleo hususan katika  Maendel...