WAZIRI ULEGA :HAKUNA SABABU YA KURUHUSU WATU WACHACHE KUVURUGA AMAN NA UTULIVU WA NCHI YETU.
Na Mwandishi wetu,DmNewsonline
ARUSHA
WAZIRI wa Ujenzi, Abdallah Ulega, amewataka Watanzania kuendelea kuilinda amani na utulivu wa nchi, akisisitiza kuwa hakuna sababu ya kuruhusu watu wachache kuitumia hali hiyo kwa maslahi yao binafsi au ya wengine.
Akizungumza jijini Arusha wakati wa ukaguzi wa miradi ya miundombinu, Ulega amesema kuna baadhi ya watu wanaotamani kuona Tanzania ikiingia katika vurugu ili wapate hoja za kuwasilisha kwa wanaowaunga mkono, lakini akasisitiza kuwa hilo halitafanikiwa.
"Kuna watu wanatamani tuwe na vurugu. Tusipokuwa na vurugu wanakosa cha kusema kwa mabwana zao. Amani tuliyonayo tusiikubali itumike vibaya kwa maslahi ya watu wachache," amesema Ulega.
Ameeleza kuwa Serikali itaendelea kuhakikisha mazingira ya amani, utulivu na maendeleo yanadumishwa huku ikiendelea kutekeleza miradi ya maendeleo kwa manufaa ya wananchi.
Ulega pia ametoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Serikali katika kulinda amani, akisisitiza kuwa ndiyo msingi wa maendeleo ya kiuchumi, uwekezaji na ustawi wa Taifa. 




Comments
Post a Comment