WADAU ZAIDI YA 200 SEKTA YA AFYA KUSHIRIKI MKUTANO WA KIMATAIFA WA SNOSSA 2026 DAR
Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline DAR ES SALAAM TAASISI ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Kimataifa wa Society for Neuro-Oncology Sub-Saharan Africa (SNOSSA) 2026, utakaofanyika ijini Dar es Salaam. Mkutano huo ukitarajiwa kukutanisha wataalamu, watafiti na wadau wa sekta ya afya zaidi ya 200 kutoka ndani na nje ya Afrika kujadili maendeleo ya tiba ya magonjwa ya mfumo wa fahamu, hususan saratani za ubongo na mfumo wa fahamu. Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Mhe. Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya, amesema mkutano huo utatoa fursa ya kujadili mbinu za kisasa za kugundua mapema magonjwa ya mfumo wa fahamu, matumizi ya teknolojia za kisasa katika uchunguzi wa radiolojia, pamoja na matibabu sahihi na ya wakati. Aidha, washiriki watajadili namna ya kuboresha upatikanaji wa huduma za afya, kuimarisha ushirikiano wa kitaaluma na kuendeleza tafiti zinazolenga kuboresha huduma kwa wagonjwa. Dkt. Mpoki ameongeza kuwa kupitia mkutano ...