WADAU ZAIDI YA 200 SEKTA YA AFYA KUSHIRIKI MKUTANO WA KIMATAIFA WA SNOSSA 2026 DAR

  Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline

     DAR ES SALAAM 

TAASISI ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Kimataifa wa Society for Neuro-Oncology Sub-Saharan Africa (SNOSSA) 2026, utakaofanyika ijini Dar es Salaam.

Mkutano huo  ukitarajiwa kukutanisha wataalamu, watafiti na wadau wa sekta ya afya zaidi ya 200 kutoka ndani na nje ya Afrika kujadili maendeleo ya tiba ya magonjwa ya mfumo wa fahamu, hususan saratani za ubongo na mfumo wa fahamu.

Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Mhe. Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya, amesema mkutano huo utatoa fursa ya kujadili mbinu za kisasa za kugundua mapema magonjwa ya mfumo wa fahamu, matumizi ya teknolojia za kisasa katika uchunguzi wa radiolojia, pamoja na matibabu sahihi na ya wakati.

Aidha, washiriki watajadili namna ya kuboresha upatikanaji wa huduma za afya, kuimarisha ushirikiano wa kitaaluma na kuendeleza tafiti zinazolenga kuboresha huduma kwa wagonjwa.

Dkt. Mpoki ameongeza kuwa kupitia mkutano huo, MOI itanufaika kwa kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika nyanja za tiba, utafiti na mafunzo

Pia, wataalamu wa taasisi hiyo watapata fursa ya kujifunza kutoka kwa wabobezi wa kimataifa kuhusu mbinu bunifu za uchunguzi, matibabu na utafiti wa magonjwa ya mfumo wa fahamu.

Kwaupande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi, Dkt. Ugumba Kwikima, ambaye ni daktari bingwa na mbobezi wa uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya mfumo wa fahamu ikiwemo saratani za ubongo, amesema kongamano hilo litakuwa jukwaa muhimu la kubadilishana uzoefu, kuwasilisha matokeo ya tafiti na kujadili changamoto zinazoathiri utambuzi na matibabu ya magonjwa hayo.

Dkt. Kwikima amesema Tanzania imepewa heshima ya kuwa mwenyeji wa mkutano huo kutokana na uwekezaji mkubwa unaoendelea kufanywa na Serikali katika kuimarisha huduma za afya kupitia upatikanaji wa vifaa vya kisasa kama Cath Lab, MRI na CT Scan, pamoja na kuongezeka kwa wataalamu wa uchunguzi, upimaji na matibabu wanaoshirikiana kwa karibu na Taasisi ya Saratani ya Ocean Road   

Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

MWAKIPOSA ASHINDA NAFASI YA UWENYEKITI WA WENYEVITI WA SERIKALI YA MTAA MKOA WA DAR ES SALAAM

DKT. KIJAZI KUSIMAMIA MIRADI YA MAENDELEO JIMBO LA KOROGWE MJINI.