WAZIRI NCHENGERWA :ATAKAYESHINDWA KUENDANA NA KASI ILIYOPO ATAONDOLEWA
Waziri wa Afya Mohamed Mchengerwa ( aliyevaa kofia) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa boti mpya ya kisasa kwa ajili ya kutolea huduma ya chanjo kwa watoto waishio maeneo ya visiwani katika Halmashauri ya Kibiti Mkoa wa Pwani,hafla ya uzinduzi huo ilifanyika Aprili 29/2026 katika Bandari ya Nyamisati Na Gustaphu Haule,DmNewsonline PWANI WAZIRI wa Afya Mohamed Mchengerwa amesema kiongozi wa ambaye atasababisha kutokuwepo na dawa na vifaa tiba katika vituo vya kutolea huduma za afya vilivyopo katika eneo lake anatakiwa kujitathmini na endapo atashindwa kuendana na kasi iliyopo ataondolewa katika nafasi yake. Mchengerwa amewataja viongozi hao kuwa ni pamoja na Waganga wafawidhi wa Wilaya na timu zao, Waganga wafawidhi wa Mikoa na timu zao pamoja na Waganga wakuu wa Wilaya na Waganga wakuu wa Mikoa. Mchengerwa amesisitiza kwa mamlaka zote za sekta ya afya wakiwemo Waganga wakuu wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha hakuna mgonjwa anayekosa dawa pal...