MBUNGE MAFINGA AAGIZA TANESCO KUUNGANISHA UMEME KWA 2700
Na Mwandishi wetu ,DmNewsonline
IRINGA
MBUNGE wa Jimbo la Mafinga Mjini, Dickson Lutevelle, amelitaka shirika la umeme Tanzania Tanesco wilayani Mufindi kutatua kero ya kukatikakatika kwa umeme kwa wakazi wa kata ya Rungemba kwani imekuwa ikididimiza Uchumi wa eneo hilo Pamoja na uharibifu wa mali.
Hayo ameyasema katika ziara yake ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa vijiji vya Kitelewasi na Itimbo ambapo ameiagiza Tanesco kuhakikisha ndani ya wiki moja wanafikisha nguzo kwa gharama ya 27000, maeneo yote ambayo hayana nguzo za umeme huku akimlipia mmoja wa wananchi wa kitelewasi gharama za kufikishiwa nguzo.
Awali wananchi walitoa kero zao mbele ya mbunge wa mafinga aliyeambatana na wataalamu kutoka halmashauri hiyo na kusema umeme umekuwa ni kero kubwa katika maeneo yao kwani umekuwa ukikatika kila wakati.
Wameongeza kuwa katika Kijiji cha Kitelewasi kuna baadhi ya maeneo nguzo hazijafika na wanapofuatilia wamekuwa wikiahidiwa bila utaekelezaji kufanyika.






Comments
Post a Comment