DKT. KIJAZI KUSIMAMIA MIRADI YA MAENDELEO JIMBO LA KOROGWE MJINI.
Na Mwandishi wetu,DmNewsonline
KOROGWE_TANGA
NI Katibu Mkuu (Mstaafu) Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Katibu Mkuu (Mstaafu) Wizara ya Maliasili na Utalii, Mkurugenzi Mkuu (DG), na Kamishna wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), sio mwingine bali ni Dkt. Allan Kijazi.
Ameonesha nia ya kuendelea kuwatumikia wananchi kupitia Mhimili mwingine wa Bunge baada ya kumaliza kazi, tena iliyotukuka kwenye Mhimili wa Serikali.
Ametangaza nia kutaka kuwa Mtumishi wa Wananchi kama Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini mkoani Tanga. Ana uwezo, ni msikivu, mchapa kazi na mwenye maono.
Anafahamu maendeleo makubwa yaliyofanywa na Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ikiwemo huduma za jamii (Elimu, Afya na Maji). Lakini pia shughuli za maendeleo kwa mtu mmoja mmoja, vikundi na Taifa.
Hivyo, yeye anataka kuendeleza pale ambapo watangulizi wake wamefikia ili yeye aweze kusimamia miradi iliyopo sasa, lakini na kuweza kusemea mahitaji ya wananchi kwenye miradi iliyopo na mingine itakayoanzishwa.
Lakini Dkt. Kijazi atakuwa mbunifu katika kuhakikisha makundi yote kwenye jamii yanajitengezea fursa za ajira, huku akifuatilia miongozo ya nchi kuweza kuona maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya viwanda na uwekezaji unafanyika, na maeneo ya biashara ndogo ndogo kwa ajili ya wajasiriamali, yanatengwa na kutumika.
MAJI
Mtia nia wa ubunge Jimbo la Korogwe Mjini mkoani Tanga Dkt. Allan Kijazi amesema dhamira yake ni ya dhati kuona wananchi wa jimbo hilo wanapata maji ya uhakika.
Kwani anafahamu mipango ya Serikali ya muda mfupi na muda mrefu wa kumaliza changamoto ya maji kwenye Mji wa Korogwe na viunga vyake.
Kwani anafahamu mipango ya Serikali ya muda mfupi ya kuondoa changamoto ya upungufu waupatikanaji wa maji kwenye Mji wa Korogwe.
MIPANGO YA MUDA MFUPI YA HTM
Kufunga pampu katika pump ya Mtonga, ambapo wameongeza uzalishaji wa maji na kupunguza athari katika maeneo ya Mtonga juu, Mtonga chini, Mtonga Kati, Member na Kwamkole Kuboresha miundombinu ya kusambaza maji kwa kulaza bomba lenye urefu wa kilomita 24.9 katika Mji wa Korogwe.
Kutumia vyanzo vya visima virefu (Mbeza mawe na Majengo) na Mto Pangani kwa uzalishaji wa maji ili kuimarisha hali ya huduma ya maji katika mji wa korogwe.
Kubadili dira za maji ambazo ufanisi wake umepungua katika maeneo ya Korogwe mjini na Mombo ili kuboresha makusanyo na kupunguza upotevu wa maji.
Kushirikiana na Ofisi ya Bodi ya Maji Bonde la Pangani kutoa elimu ya utunzaji wa vyanzo vya Maji kwa maendeleo endelevu sambamba na kuweka alama katika maeneo ya vyanzo vya maji.
MPANGO WA MUDA MREFU YA HTM
Mipango ya muda mrefu ni
Ujenzi wa mradi wa maji kwa kutumia chanzo cha Mto Ndemaha, ambapo linajengwa dakio, kulaza bomba kuu lenye urefu wa kilomita 21 Kutekeleza ujenzi wa tenki la kuhifadhia maji lenye uwezo wa kujaza lita 2,000,000 eneo la Kwamkole.
Kutekeleza ujenzi wa Nyumba ya Maabara na vifaa vyake (Laboratory House & Laboratory Facilities) katika eneo la Kwamkole Kutekeleza ujenzi wa miundombinu ya kusafisha, kuchuja na kutibu maji (Water Treatment Plant) katika maeneo ya Mji wa Korogwe na Mji mdogo wa Mombo kwa ajili ya kuhakikisha maji yanawafikia wananchi yakiwa safi na salama tofauti na ilivyo hivi sasa.
• Utekelezaji wa mradi wa Upanuzi na ukarabati wa mtandao wa mabomba katika mji mdogo wa Mombo ili kuboresha huduma ya maji Utekelezajiwa mradi wa Miji 28 ambapo Mji wa Korogwe ni moja ya miji itakayonufaika na mradi huo
Hadi sasa mkandarasi yuko eneo la mradi anaendelea na ujenzi katika maeneo mbalimbali ya mradi ambapo anaendelea na Ujenzi wa dakio la maji (Water intake), Ujenzi wa Chujio (Water Treatment
Plant), Ulazaji wa mabomba ambapo mpaka sasa amelaza jumla ya km 164.84 kati ya km 188 na Ujenzi wa matenki 8 katika maeneo tofauti.
BARABARA ZA MJI WA KOROGWE
Kijazi anajua kuna utekelezaji wa miradi yabarabara za Mji wa Korogwe kupitia Mradiwa Miji ya Tanzania kwa Mageuzi ya Miundombinu na Uboreshaji wa Ushindani(TACTIC), ambapo kwa fedha hizo kutajengwa barabara kwa kiwango cha lami kutoka njiapanda ya Handeni eneo la Bagamoyo kupitia Mgombezi hadi Kibo, Mtonga yenye urefu wa kilomita 6.7.
Barabara nyingine ni ile ya kutoka Benki ya NMB hadi Hospitali ya Magunga yenye urefu wa kilomita 2.7. Pia barabara ya kuzunguka Mahakama mpya ya Wilaya ya Korogwe, Soko jipya la Kilole na kurudi njia ya Handeni yenye urefu wa zaidi ya kilomita moja, hivyo kufanya barabara zitakazojengwa kwenye mpango huo wa TACTIC kuwa za kilomita 10.2
TARURA ambao ndiyo Wasimamizi wa barabara za miji, wamepanga kununua taa mpya za barabarani, na kwa mwaka wa fedha 2025/2026, wamepanga kununua taa 20 kutoka eneo la bar ya Mountain View hadi barabara ya kutoka Mti mkubwa hadi kwa Majimarefu.
Pia kwa bajeti ya mwaka wa fedha 2026/2027 kutawekwa taa barabara ya kutoka kwa Sheikh Ramia hadi KKKT, na kutoka Mti mkubwa hadi kwa Majimarefu. Na taa zote hizo itakuwa sio za betrii, sababu nyingi ya taa za aina hizo zimekufa baada ya watu kuiba betrii.

Comments
Post a Comment