Posts

Showing posts from July, 2026

MCHANGE AHOJI: DK. NCHIMBI ANAJUA MADHARA YA KAULI ZAKE AU ANATUTEGA?

Image
Na Mwandishi Wetu,DmNewsTz Mchambuzi wa masuala ya siasa, jamii na maendeleo, Habibu Mchange, ametoa tafakuri kuhusu utata wa kauli za mara kwa mara za Makamu wa Rais, Dk. Emmanuel Nchimbi, akisema kutokana na nafasi yake ya kikatiba kama Msaidizi Mkuu wa Rais kwa mujibu wa Ibara ya 47(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kauli zake zinapaswa kupimwa kwa uzito mkubwa kwa kuwa zina athari kwa Serikali, mshikamano wa uongozi na imani ya wananchi kwa taasisi za dola. Katika tafakuri hiyo yenye kichwa "DK. NCHIMBI ANAJUA MADHARA YA KAULI ZAKE AU ANATUTEGA?", Mchange amechambua kauli ya Dk. Nchimbi kwamba "Katiba iliyopo ina mapungufu na inampa Rais madaraka yasiyo na maana," pamoja na wito wake wa "komaeni, pambaneni mpate Katiba mpya," akisema kauli hizo zimezua mjadala mkubwa wa kikatiba na kisiasa, hasa wakati Serikali tayari imeeleza kuwa mchakato wa Katiba mpya utaanza baada ya kukamilika kwa maridhiano ya kitaifa.  Amehoji kuwa iwapo Serikali...

DC NZEGA ATOA OFA YA ELIMU KWA WATOTO WASIO NA UWEZO

Image
  Na Allan Kitwe,DmNewsonline                   TABORA WILAYA ya Nzega Mkoani Tabora imetangaza ofa ya elimu kwa watoto wote wanaochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza na wale wanaochaguliwa kuingia kidato cha tano watakaoshindwa kuripoti shuleni kwa kukosa mahitaji muhimu. Ofa hiyo imetangazwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Naitapwak Tukai alipokuwa akiongea na wananchi kwenye ziara ya Kamati ya Siasa iliyotembelea na kukagua mradi wa shule mpya ya Sekondari ya Kampala iliyopo katika Kata ya Ndala. Amesema kuwa shule hiyo iliyogharimu zaidi ya shilingi milioni 300 imekamilika kwa asilimia 100 na imejengwa kwa ubora wa hali ya juu, hali itakayosaidia watoto kusomea kwenye shule yenye mazingira bora zaidi.       Mkuu huyo wa Wilaya  amesisitiza kuwa wamejipanga vizuri ili kuhakikisha watoto wote wanaochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza na wale wanaochaguliwa kuendelea kidato cha tano wanaripoti katika shule zao pasipo kuk...

WAKALA MKUU WA ASA MKOA WA IRINGA AWAHIMIZA WAKULIMA KUTUMIA MBEGU BORA KUONGEZA MAVUNO

Image
 Na Eliasa AllyDmNewsonline                      IRINGA WAKALA Mkuu wa mbegu za Taasisi ya ASA mkoani Iringa, Kampuni ya Mgongolwa Agrovet & Seeds Company Limited, imewahimiza wakulima kutumia mbegu bora zinazozalishwa na Taasisi ya ASA ili kuongeza uzalishaji wa mazao na kuondokana na changamoto ya kutumia mbegu zisizo na ubora. Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Iringa Press Club, Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Joseph Saidi Mgongolwa, alisema wamepewa dhamana na Taasisi ya ASA iliyo chini ya Wizara ya Kilimo kuhakikisha mbegu bora zinawafikia wakulima wa vijijini na mijini kwa wakati kabla ya kuanza kwa msimu wa kilimo. Amesema hatua hiyo ni sehemu ya maandalizi kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wakulima (Nanenane), huku lengo likiwa kuwafikishia wakulima mbegu zenye ubora wa hali ya juu kwa bei nafuu ili kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao. Mgongolwa amesema Taasisi ya ASA imeamua kusogeza huduma karibu n...

PROTECTING OUR CHILDREN TODAY WILL SHAPE THEIR FUTURES TOMORROW ‎

Image
‎Dar es Salaam, Tanzania Africa has the youngest population in the world with more than 400 million young people aged between the ages of 15 to 35 years. This is a generation filled with potential and the power to shape the continent’s future. Yet, for millions of children across malaria-endemic regions, repeated malaria infections continue to interrupt childhood at some of its most important stages. ‎According to research, malaria disproportionately affects children in Tanzania, highlighting their vulnerability to infection. The predominance of P. falciparum mixed infections indicates the complex epidemiology in the country. The high burden in Lake zones stresses the need for new interventions. ‎Experts warn that malaria’s long-term impact on children’s futures deserves more attention. ‎“Malaria does not only affect health in the moment,” says Brian Tarimo, Principal Research Scientist at Ifakara Health Institute (IHI) and a Lead Scientist at the Transmission Zero (T0) programme, an...

UYUI YAANZISHA MIRADI KUCHOCHEA KASI YA MAENDELEO

Image
Na Allan Kitwe, DmNewsonline                TABORA   HALMASHAURI ya Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora imedhamiria kuongeza mapato zaidi kupitia vyanzo vyake vya ndani kwa kuanzisha miradi ya kimkakati ili kuchochea kasi ya maendeleo ya wananchi. Hayo yamebainishwa jana na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Shaban Katalambula ambaye ni diwani wa Kata ya Goweko alipokuwa akitoa taarifa ya miradi ya halmashauri kwa Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa. Amesema kuwa licha ya kuwa na vyanzo kadhaa vya mapato halmashauri imeanza kutekeleza mradi mkubwa wa ujenzi wa vibanda vya biashara katika eneo la stendi ya mabasi ambavyo vitakavyokodishwa kwa wananchi. ‘Mradi huu utakaogharimu kiasi cha shilingi milioni 74 unatarajia kuongeza  mapato ya halmashauri kwa kiasi kikubwa hivyo kuchochea kasi ya utekelezaji miradi ya maendeleo kwa manufaa ya wananchi’, ameeleza. Amedokeza kuwa halmashauri imeendelea kupiga hatua kubwa kimaendeleo na kupata mafanikio makubw...

WALIMU SIKONGE WAPEWA ELIMU YA MALEZI BORA

Image
     Na Allan Kitwe, DmNewsonline                  Tabora WALIMU Wilayani Sikonge Mkoani Tabora wametakiwa kufanya kazi kwa weledi na kulea wanafunzi katika maadili yanayofaa ili watakapomaliza masomo wawe na tabia njema miongoni mwa jamii. Aidha wametakiwa kuzingatia miongozo na taratibu zilizowekwa na serikali katika kutekeleza majukumu yao ili kuongeza ufanisi katika utoaji huduma za elimu kwa watoto wawapo shuleni. Wito huo umetolewa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Selemani Pandawe alipokuwa akifungua mafunzo ya malezi na unasihi kwa walimu na wanafunzi yanayoratibiwa na Shirika la UNICEF Wilayani hapa. Pandawe amesisitiza kuwa walimu wanapaswa kuacha tabia ya kufanya kazi kwa mazoea na kubahatisha, bali wazingatie taratibu, sheria na miongozo inayotolewa na Wizara ya Elimu ili wanafunzi walelewe katika njia zinazofaa. ‘Mwalimu unapopata jambo lolote mezani kwako huna haja ya kutafuta ufumbuzi...

URAMBO WAFURAHIA MRADI WA KUPUNGUZA VIFO VYA WATOTO

Image
Na Allan KitweDmNewsonline                    URAMBO  WANANCHI Wilayani Urambo  Mkoani Tabora wameeleza kufurahishwa na uamuzi wa Serikali ya Awamu ya Sita kupeleka zaidi ya shilingi mil 660 kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa kupunguza vifo vya watoto wachanga. Akizungumza mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa waliokuwa katika ziara ya siku moja Wilayani humo jana Mbunge wa Jimbo hilo Magreth Sita ameeleza kuwa mradi huo utasaidia sana kupunguza vifo vya watoto wachanga. ‘Tunamshukuru sana Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea kiasi hicho ili kujengwa mradi utakaohudumia watoto wa changa (NICU) katika Wilaya yetu’, ameeleza. Amefafanua manufaa mengine ya mradi huo kuwa ni kusogeza huduma za afya ya mtoto karibu zaidi na wananchi na kupunguza rufaa za kwenda Hosptali ya Mkoa. Faida nyingine ni kuboreshwa huduma za afya kwa watoto wachanga wakiwemo waliozaliwa njiti, wenye ulemavu, wenye matatizo ya kupumua na ya kimaumbi...

MWENYEKITI WAZAZI TAIFA CCM AWAASA VIONGOZI PWANI.

Image
Na Mwandishiwetu,DmNewsOnline                         KIBAHA    MWENYEKITI Jumuiya wazazi Taifa  Fadhili Maganya amewaasa Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi  (CCM)  ngazi  za Wilaya pamoja na   Mkoa wa Pwani  kuhakikisha kwamba  wanalivalia njuga  suala la kero  ya  migogoro ya ardhi sambamba na kusikiliza   changamoto zinazowakabili wananchi na kuzitafutia ufumbuzi. Kauli hiyo ameitoa wakati wa ziara yake ya  kikazi yenye lengo la kukijenga Chama pamoja na kuangalia uhai wake  pamoja na kuimarisha Jumuiya zake, na kuangalia mwenendo mzima wa utekelezaji wa ilani  ya CCM na  kukagua miradi mbali mbali  ya maendeleo. Mwenyekiti huyo  amebainisha kuwa katika ziara hiyo pia imelenga kukutana na viongozi mbali mbali wa serikali na kupokea taarifa zao  zinazohusiana  na suala zima la  utekelezaji wa kazi  zao...

SHULE YA ELIMU MAALUMU SIKONGE YABORESHWA

Image
  Na Allan Kitwe, DmNewsonline              TABORA  SERIKALI imepeleka zaidi ya shilingi milioni 100 Wilayani Sikonge Mkoani Tabora ili kuifanyia maboresho makubwa miundombinu ya shule ya msingi Sikonge inayotoa elimu maalumu kwa watoto wenye ulemavu. Miundombinu ya shule hiyo yenye watoto 144 (wavulana 92 na wasichana 52), iliyoanzishwa mwaka 2011 Wilayani humo ilikuwa imechakaa sana hali iliyopelekea mazingira yake kutokuwa rafiki kwa watoto wenye mahitaji maalumu. Akitoa taarifa ya shule kwa Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Seleman Pandawe, Katibu wa Kamati ya Ujenzi Makanika Kajuni ameishukuru serikali kwa kuwapatia fedha hizo. Ameeleza kuwa walipokea kiasi cha shilingi mil 112.2 mwezi Julai 2025 ambazo zimewezesha kujengwa vyumba 4 vya madarasa ya kisasa, kukarabati miundombinu iliyochakaa ikiwemo uzio na geti, kwa sasa shule inang’aa. Mbunge wa Jimbo la Sikonge, Mhandisi Amos Magang...

DHAHABU YA KILOGRAMU 4.4 YAKAMATWA PWANI

Image
Na Timothy Marko,DmNewsOnline                             DAR ES SALAAM:  SERIKALI  imefanikiwa kukamata dhahabu yenye uzito wa kilogramu 4.4 iliyokuwa ikitoroshwa katika eneo la Kiluvya, Mkoani Pwani. Akizungumza leo, Julai 27, 2026,Jijini Dar es Salaam, Waziri wa Madini, Antony Mavunde, amesema tukio hilo la utoroshaji wa dhahabu  limetokea Julai 25, mwaka huu Kiluvya Pwani. Amesema dhahabu hiyo yenye thamani ya shilingi milioni 108.87 ili sababisha Serikali kukosa mapato yanayotokana na kodi yanayokadiriwa kufikia shilingi milioni 100. “Serikali ina vituo vya uuzaji wa Madini takribani 107 na Masoko 47 ya uuzaji wa madini,” amesema Mavunde. Ameongeza kuwa mtu anayefanya biashara ya madini anatakiwa kuwa na leseni inayotolewa na Wizara ya Madini. Waziri Mavunde pia amesema hadi kufikia Juni 30, mwaka huu, Wizara ya Madini imefanikiwa kuchangia mapato ya Serikali yanayofikia takribani shilingi trilioni...