Posts

Showing posts from March, 2026

TAMISEMI YAWASILISHA RANDAMA YA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI

Image
Leo Machi 31, 2026, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI), Mhe. Prof. Riziki Shemdoe, amewasilisha randama ya makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2026/27. Mhe. Prof. Shemdoe amewasilisha randama hiyo yenye mafungu 37 kwa niaba ya Waziri Mkuu, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba ambaye anatarajia kusoma rasmi makadirio hayo kesho tarehe 01 Aprili, 2026 katika kikao cha pili cha mkutano wa tatu wa Bunge la Bajeti, ambapo Wabunge watapata fursa ya kujadili mipango na matumizi ya fedha ya ofisi hiyo.

PROFESA MAPESA AZINDUA MBAO JANJA (SMART BOARD) KUENDANA NA TEKNOLOJIA

Image
  Na Mwandishi wetu,DmNewsonline                    DAR ES SALAAM  MKUU wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Profesa Haruni Mapesa leo amezindua Mbao janja (Smart board) zinazotumika kwa ajili ya kufundishia ambapo amesema kutokana na Mabadiliko ya Kielektroniki matumizi ya vifaa  kama Smart board ni lazima ili kuendana na Sayansi na Teknolojia. Prof. Mapesa amesema ni lazima wanataaluma wakubaliane na Mabadiliko ya kiteknolojia katika matumizi ya kufundishia, kuelekeza na kujifunzia na kuwa kila mmoja awe sehemu ya mpango huo na kuwa kuwepo kwa mbao janja hizo kutasaidia kuendesha Semina na kufanyika kwa Mihadhara kwa wadau wengi kwa wakati mmoja bila kujali umbali. Mkuu huyo wa Taasisi amewapongeza Wanataaluma kwa utekelezaji wa Majukumu yao ikiwemo uvumilivu, na kusema kuwa kazi ya kufundisha ni wito na ina wajibu mkubwa, hivyo Mbao Janja hizo 21 zitasaidia Chuo kuendana na Teknolojia Akizungumza kabla ya Kumkaribi...

SERIKALI YAITAKA NEMC KUHAKIKISHA UZALISHAJI WA TAKA UNATOKOMEZWA IFIKAPO 2027.

Image
     Timothy Marko DmNews Online                 DAR ES SALAAM  KATIKA kuhakikisha tatizo la Uzalishaji wa taka linatokomezwa Nchini,Serikali  imewataka Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kuhakikisha wanatoa mafunzo juu ya Uhifadhi wa Mazingira ili kufikia lengo la taka sifuri ifikapo 2027. Akizungumza leo March 30 ,2026 jijini Dar es Salaam Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhandisi Hamad Masauni amesema ili kuweza kufikia malengo hayo Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan ametoa miongozo Mbalimmbali ikiwemo Uhamasishaji wa Nishati  safi yakupikia. "Pia Rais Dk.Samia Suluhu Hassan anahamasisha upandaji miti ilikuweza fikia Dira ya Maendeleo 2050"Amesma Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Mhandisi Hamadi Masauni. Mhandisi Masauni Ameongeza kuwa ilikuweza kufikia Malengo ya Uzalishaji wataka sifuri Mhandisi Masauni amezitaka taasisi za Elimu N...

VIJANA 521 WANAOKWENDA KUFANYA KAZI NJE YA NCHI WAHAKIKISHIWA USALAMA WAO

Image
  Na Mwandiahi wetu,DmNewsOnline      DAR ES SALAAM  SERIKALI imejipanga kuhakikisha usalama wa Watanzania wanaokwenda kufanya kazi nje ya nchi wanalindwa kikamilifu, na kuwahakikishia vijana hao kuwa waende kwa utulivu na kujiamini kwa kuwa Serikali ipo pamoja nao. Akizungumza katika hafla ya kuwaaga vijana 521 waliopata fursa za ajira nje ya nchi, iliyofanyika Machi 27, 2026 jijini Dar es Salaam, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu -Kazi, Ajira na Mahusiano, Mheshimiwa Deus Sangu, alisema hatua hiyo ni utekelezaji wa maono ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kukuza ajira kwa vijana Serikali imeendelea kufungua na kuimarisha njia salama za uhamiaji wa nguvu kazi kwa kushirikiana na nchi rafiki pamoja na taasisi za kikanda na kimataifa,ikiwa ni juhudi za kuhakikisha Watanzania wanapata ajira zenye staha, kulindwa haki zao na kushiriki kikamilifu katika uchumi wa dunia. .Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kitengo cha Ajira, Bi. Jane Sologo, aliwashukuru mawakala bina...

The Brutality and Atrocities of Sudan’s Rebels: Will the World Choose Silence or Stand Up to Fight for Peace?

Image
         By M oses Ntandu, Dar es Salaam,                                Tanzania Without shame or considering of human dignity and the rights of innocent civilians, the Rapid Support Forces (RSF) rebels in Sudan continue to raid civilian homes, carrying out killings, looting property, and committing numerous human rights violations in several areas in the country. These actions carried out by the RSF rebels must not be met with silence at all, as they continue to harm countless innocent civilians while grave human rights violations persist and the world watches as if nothing is happening. No, this is not right at all!! The world should stand firm in defending human dignity, what is happening in Sudan ought to awaken the conscience of every one of us. The tears of innocent civilians, the cries of children who have lost their families, and the fear that dominates daily life—these are ...

RAIS DKT.SAMIA AMESEMA TAIFA LIMEPOTEZA KIONGOZI MAHILI NA MZALENDO WA KWELI KWA NCHI YAKE ,ATOA POLE KWA FAMILIA .

Image
. Na Mwandishi wetu,DmNewsonline                DAR ES SALAAM RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan leo Machi 28 ,2026 amewaongoza watanzania na viongozi mbalimbali kutoa salamu za mwisho katika viwanja vya kamrimjee jijini Dar es salaam katika msiba wa aliyekuwa Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu Bunge ,Sera ,uratibu na watu wenye ulemavu marehemu William Lukuvi. Rais.Dkt Samia akizungumza wakati Akitoa heshima zake za mwisho kabla ya kwenda kumpumzisha kijijini kwao mkoani iringa amesema kuwa Taifa limepoteza kiongozi muhimu. Amesema William Lukuvi alikuwa kiongozi aliyelitumikia Taifa kwa muda mrefu na alikuwa kiongozi mwenye kijtuma na mzalendo wa kweli katika nchi yake. Pia Rais Dkt. Samia ametumia hadhara hiyo kutoa pole kwa familia na kuwasihi kuwa na subira hasa katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao marehemu  William Lukuvi. Marehemu Waziri Lukuvi alifariki Dunia Machi 25, katika Hospitali...

MTOTO MCHANGA ACHINJWA,TABORA

Image
 Na Allan Kitwe,DmNewsonline                  IGUNGA  MWANAUME mmoja mkazi wa Kijiji cha Imalanguzu, Kata ya Mwamakona, Tarafa ya Igurubi, Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora amemchinja mtoto wake mchanga aliyekuwa na umri wa miezi miwili na kumjeruhi vibaya mke wake. Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo, Kamanda wa Polisi Mkoani hapa , Richard Abwao ameeleza kuwa tukio hilo limetokea Machi 25 mwaka huu majira ya saa 3 usiku huko katika Kitongoji cha Ibindo, kijiji cha Imalanguzu. Amebainisha kuwa mwanaume aitwaye Bunzali Jidola (30) Msukuma, mkulima, mkazi wa Imalanguzu alimchinja kwa kutumia kitu chenye ncha kali mtoto wake aitwaye Dorcas Bunzali aliyekuwa na umri wa miezi miwili. Ameongeza kuwa baada ya mauaji hayo alimjeruhi pia mke wake aitwaye Jeni Ndaki (24) Msukuma, mkulima, mkazi wa Kijiji cha Ibutamisuzi kwa kutumia kifaa hicho chenye ncha kali na kisha kutokomea kusiko julikana. Amesema majeruhi huyo aliokolewa na wasamari...

VIJANA ZAIDI YA 60 WALIOHITIMU FDC NZEGA WAPATA AJIRA

Image
  Na Allan Kitwe, DmNewsonline               NZEGA TAASISI, Mashirika ya Umma na makampuni binafsi yamepongezwa kwa kutoa fursa za ajira kwa vijana wa kike na kiume wanaohitimu mafunzo ya ufundi katika fani mbalimbali kwenye Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi (FDC) . Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Chuo Cha Maendeleo ya Wananchi Nzega (Nzega FDC) Nichodemus Shirima alipokuwa akiongea na waandishi wa habari waliomtembelea Ofisini kwake jana ili kujionea maendeleo ya chuo hicho. Ameshukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuvifanyia maboresho makubwa vyuo vyote vya maendeleo ya wananchi nchini na kuvipatia vifaa vya kutosha vya kufundishia na kujifunzia hali ambayo imechochea vyuo hivyo kutoa elimu bora. ‘Zaidi ya vijana sitini (60) waliohitimu fani mbalimbali katika chuo chetu hapa Nzega wamepata ajira rasmi katika taasisi mbalimbali za umma na makampuni ya watu binafsi na wengine wamejiajiri na wanapata kipato cha uhakika’, ameeleza. Shirima amefafanua vij...

UNFPA NA WADAU WAKUTANA KUJADILI JINSI YA KUIMARISHA UKATILI WA KIDIJITALI DHIDI YA WANAWAKE NA WASICHANA

Image
Na Angelina Mganga,DmNewsOnline                DAR ES SALAAM  UKATILI wa Kijinsia  umekuwa mojawapo ya changamoto kubwa za haki za binadamu nchini Tanzania .huku takwimu za kitaifa zinaonyesha  kuwa asilimia 39.5 ya wakefu wenye umri wa miaka 15 hadi 49 wamekumbwa na ukatili wa kimwili,kihisia au kingono kutoka kwa wapenzi wao kiwango kilichozidi wastani wa Dunia na Kanda  pamoja na ongezeko la haraka la upatikanaji wa mitandao karibu. Jumla  watumiaji milioni 29 mwaka 2023 ukitishi wa kidigitali umekua na kuenea zaidi katika nafasi za mtandaoni . Akizungumza katika  mkutano wa huo uliofanyika Machi 26,2026 Jijini Dar es Salaam Naibu Mwakilishi na Kaimu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Melisa Mcnell Barret amesema kuwa UNFPA kwa kushirikiana na C-Sema chini ya Mpango wa Chaguo Langu Haki Yangu,kwa msaada wa kifedha kutoka Finland umewakutanisha wataalam wa kitaifa na kimataifa kupitia uchambuzi wa ushahidi,mapitio ya sera ...

𝐙𝐈𝐌𝐄𝐒𝐀𝐋𝐈𝐀 𝐒𝐈𝐊𝐔 𝐂𝐇𝐀𝐂𝐇𝐄 𝐊𝐔𝐅𝐈𝐊𝐈𝐀 𝐔𝐊𝐎𝐌𝐎 𝐖𝐀 𝐓𝐀𝐀𝐒𝐈𝐒𝐈 𝐊𝐔𝐉𝐈𝐒𝐀𝐉𝐈𝐋𝐈 𝐏𝐃𝐏𝐂

Image
  Na Mwandishi wetu,DmNewsonline                    DODOMA  ZIMESALIA  siku chache kabla ya kufikiwa kwa ukomo wa usajili wa hiari kwa taasisi zinazokusanya na kuchakata taarifa binafsi nchini. Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) imetangaza kuwa ifikapo tarehe 9 Aprili mwaka huu, itaanza kuchukua hatua kali za kisheria ikiwemo faini ya hadi shilingi bilioni tano kwa taasisi zitakazokiuka taratibu hizo. Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) leo Machi 26, 2026 imetoa msisitizo wa mwisho kwa taasisi zote za umma na binafsi nchini, ikizikumbusha kuwa muda wa usajili wa hiari unafikia tamati tarehe 8 Aprili, 2026. Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo, Dkt. Emmanuel Lameck Mkilia, amesema kuwa serikali imetoa muda wa kutosha tangu mwaka 2024 ili kutoa fursa kwa taasisi kujipanga. “Serikali ilitoa muda wa kutosha wa kujisajili. Muda huo ulianza Aprili 2024 wakati Rais wa Jamhuri ...