UNFPA NA WADAU WAKUTANA KUJADILI JINSI YA KUIMARISHA UKATILI WA KIDIJITALI DHIDI YA WANAWAKE NA WASICHANA

Na Angelina Mganga,DmNewsOnline

               DAR ES SALAAM 

UKATILI wa Kijinsia  umekuwa mojawapo ya changamoto kubwa za haki za binadamu nchini Tanzania .huku takwimu za kitaifa zinaonyesha  kuwa asilimia 39.5 ya wakefu wenye umri wa miaka 15 hadi 49 wamekumbwa na ukatili wa kimwili,kihisia au kingono kutoka kwa wapenzi wao kiwango kilichozidi wastani wa Dunia na Kanda  pamoja na ongezeko la haraka la upatikanaji wa mitandao karibu.

Jumla  watumiaji milioni 29 mwaka 2023 ukitishi wa kidigitali umekua na kuenea zaidi katika nafasi za mtandaoni .

Akizungumza katika  mkutano wa huo uliofanyika Machi 26,2026 Jijini Dar es Salaam Naibu Mwakilishi na Kaimu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Melisa Mcnell Barret amesema kuwa UNFPA kwa kushirikiana na C-Sema chini ya Mpango wa Chaguo Langu Haki Yangu,kwa msaada wa kifedha kutoka Finland umewakutanisha wataalam wa kitaifa na kimataifa kupitia uchambuzi wa ushahidi,mapitio ya sera na utambuzi wa hatua za vitendo za kuzuia na kupambana na ukatili wa kijinsia unaotokea kwa kutumia teknolojia nchini Tanzania.
.
Aidha ,amesema mkutani huo umewakutanisha taasisi za kiserikali,washirika wa maendeleo,mashirika ya kiraia,wadau wa teknolojia na wawakilishi wa vijana unaohusu Viashiria vya ukatili wa kijinsia vinavyofanyika kupitia Teknolojia dhamira ni kuimarisha majibu ya Tanzania dhidi ya ongezeko la ukatili wa kidijitali dhidi ya wanawake na wasichana.

Hata hivyo,Melisa Barret ameeleza kuwa teknolojiq inapaswa kiwa chombo Cha kuwawezesha watu badala kuwa jukwaa la kuumiza .

"Kadri upatikanaji wa intanetu unavyozidi kuomgezeka ni lazima kuwepo na hatua madhubuti za kuhakikisha wanawake na wasichana wanatumiq nafasi za kidijitali kwa usalamabila hofu ya kunyanyaswa,ni muhimu kutumia ubunifu wa kidijitali kwa ajili ya kuleta usawa wa kijinsia na ulinzi wa hakibza binadamu",amesema Melisa.

 Naye Balozi wa Finland nchini Tanzania Theresa Zitting ameeleza kuwa ushirikiano uliopo kati ya serikali ya Finland,UNFPA  na serikali ya  Tanzania wamejizatiti kushirikiana na wataalamu wa kimataifa katika maenei ya utawala wa kidijitali usalama wa mtandao na matumizi ya teknolojia  yenye juhudi zakuhakikisha maendeleo ya teknolojia yanachangia kukuza usawa wa kijinsia badala yakuongeza pengo la ukatili

Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

DKT. KIJAZI KUSIMAMIA MIRADI YA MAENDELEO JIMBO LA KOROGWE MJINI.