MWAKIPOSA ASHINDA NAFASI YA UWENYEKITI WA WENYEVITI WA SERIKALI YA MTAA MKOA WA DAR ES SALAAM
Na Angelina Mganga -DmNewsOnline
BDAR ES SALAAM
UCHAGUZI wa nafasi ya Uwenyekiti na Katibu Mkuu wa Umoja wa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam umefanyika Leo Juni 20,2026,na umemalizika kwa amani na utulivu.
Uchaguzi huo ulikuwa na wagombea watatu ambao wamewania nafasi hiyo ya Uwenyeviti wa Wenyeviti wa Serikali ya Mtaa Mkoa wa Dar es Salaam
Wagombe wa nafasi ya Uwenyeviti ni Consolatha M.Rwiza Juma A.Mwingano na Razalous A.Mwakiposa
Katika uchaguzi huo Razalous A.Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi hiyo ya
Uwenyekiti huku Peppino Sudi Peppino akishinda nafasi ya Katibu.
Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo,Msimamizi wa Uchaguzi Kambi Sinde amesema kuwa kura zilizopigwa ni 37 na wagombea walikuwa Consolatha M.Rwiza (11),Juma A.Mwingano (2 )na Razalous A.Mwakiposa ( 24 ) hakuna kura iliyoharibika.
Razalous A.Mwakiposa ameshinda Kwa kura 24 kati ya kura 37zilizopigwa huku Katibu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa.
Wajumbe waliohudhuria katika uchaguzi huo 37 kutoka Wilaya ya Temeke (5),Kigamboni(8)Ubungo(8),Ilala(7) na Kinondoni(7) ambapo wajumbe wote walitakiwa kuwa Wajumbe 40 lakini walioshoriki ni 37 tu na watatu walitoa udhuru.
"Uchaguzi umefanyika wa haki na uwazi ",amesema
Kwa upande wa nafasi ya Katibu wagombea walikuwa wawili ambao ni Athumani S.Gereza na amepata kura 17 huku Peppino Sudi Peppino akijinyakulia kura 20.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutangazwa mshindi kwenye uchaguzi huo,Mwenyekiti Mpya wa Uwenyeviti wa Serikali ya Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam,Razalous A.Mwakiposa amewashukuru wajumbe wa umoja huo kwa kumchagua na kimwamini kuwa kiongozi wao,hivyo ameahidi kufanya kazi kwa ushirikiano pamoja na kuhakikisha anapigania maslahu ya wenyeviti wa Serikali Mitaa ili waweze kulipwa posho ama mishahara inayokidhi mahitaji Yao,kwani wenyekiti wanatumia muda mwingi kuwahudumia wananchi.
"Tunamuomba Mama yetu Rais Dkt
Samia Suluhu Hassan atukumbuke watoto wake tulipwe posho zitakazokidhi mahitaji yetu ili tufanye kazi kwa ufanisi",alisema Mwakiposa
Aidha,amesema kuwa atashirikiana na wenyeviti wote wa Mkoa wa Dar es Salaam kuhakikisha vikundi vya ulinzi shirikishi vinakuwepo Kila mtaa ili viweze kulinda usalama ili kuepukana na vitendo vya uhalifu.
Naye Katibu wa Wenyeviti wa Serikali ya Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam,Peppino Sudi Leppino amesema atashirikiana na Mwenuekiti pamoja na wenyeviti wote wa Mkoa ili kuhakikisha umoja huo unatimiza malengo waliyojiwekea. 


Comments
Post a Comment