RAIS DKT.SAMIA AMESEMA TAIFA LIMEPOTEZA KIONGOZI MAHILI NA MZALENDO WA KWELI KWA NCHI YAKE ,ATOA POLE KWA FAMILIA .

. Na Mwandishi wetu,DmNewsonline 

              DAR ES SALAAM

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan leo Machi 28 ,2026 amewaongoza watanzania na viongozi mbalimbali kutoa salamu za mwisho katika viwanja vya kamrimjee jijini Dar es salaam katika msiba wa aliyekuwa Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu Bunge ,Sera ,uratibu na watu wenye ulemavu marehemu William Lukuvi.

Rais.Dkt Samia akizungumza wakati Akitoa heshima zake za mwisho kabla ya kwenda kumpumzisha kijijini kwao mkoani iringa amesema kuwa Taifa limepoteza kiongozi muhimu.

Amesema William Lukuvi alikuwa kiongozi aliyelitumikia Taifa kwa muda mrefu na alikuwa kiongozi mwenye kijtuma na mzalendo wa kweli katika nchi yake.

Pia Rais Dkt. Samia ametumia hadhara hiyo kutoa pole kwa familia na kuwasihi kuwa na subira hasa katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao marehemu  William Lukuvi.

Marehemu Waziri Lukuvi alifariki Dunia Machi 25, katika Hospitali ya Benjamini Mkapa iliyopo jijini Dodoma alipokuwa anapatiwa matibabu. 

Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

DKT. KIJAZI KUSIMAMIA MIRADI YA MAENDELEO JIMBO LA KOROGWE MJINI.