SERIKALI YAITAKA NEMC KUHAKIKISHA UZALISHAJI WA TAKA UNATOKOMEZWA IFIKAPO 2027.

 
   Timothy Marko DmNews Online 

               DAR ES SALAAM 

KATIKA kuhakikisha tatizo la Uzalishaji wa taka linatokomezwa Nchini,Serikali  imewataka Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kuhakikisha wanatoa mafunzo juu ya Uhifadhi wa Mazingira ili kufikia lengo la taka sifuri ifikapo 2027.

Akizungumza leo March 30 ,2026 jijini Dar es Salaam Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhandisi Hamad Masauni amesema ili kuweza kufikia malengo hayo Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan ametoa miongozo Mbalimmbali ikiwemo Uhamasishaji wa Nishati  safi yakupikia.

"Pia Rais Dk.Samia Suluhu Hassan anahamasisha upandaji miti ilikuweza fikia Dira ya Maendeleo 2050"Amesma Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Mhandisi Hamadi Masauni.

Mhandisi Masauni Ameongeza kuwa ilikuweza kufikia Malengo ya Uzalishaji wataka sifuri Mhandisi Masauni amezitaka taasisi za Elimu Nchini ikiwemo Shule za Msingi na Secondari kuhamasisha Uhifadhi wa Mazingira. 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uhifadhi wa Mazingira NEMC  immaculate Semesi amesema kuwa ili kufikia Uzalishaji wataka sifuri Serikali imeweka miongozo ikiwemo matumizi ya Sheria na kupunguza Uzalishaji wa taka zitokanazo na chakula.
Amesema Taasisi hiyo imeweka mifumoya kubadili taka kuwa mbolea.

"Sambamba na hilo,NEMC imeweka mafunzo ya kubadili mitazamo na utamaduni wa taka kuwa fursa" Amesema immaculate Semesi. 
.

Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

DKT. KIJAZI KUSIMAMIA MIRADI YA MAENDELEO JIMBO LA KOROGWE MJINI.