VIJANA WA DENMARK WASHIRIKI MSALAGAMBO KOROGWE
Meneja wa TFCG Wilaya ya Korogwe Bettie Luwuge (katikati) akizungumza na wakulima wa Vugiri. Na Yusuph Mussa, DmNewsonline KOROGWE VIJANA sita kutoka nchini Denmark wameshiriki kilimo cha msalagambo (pamoja) na wakulima wa mahindi., maharage na mbogamboga wa Kijiji cha Vugiri, Kata ya Vugiri, Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga. Pamoja na mambo mengine, vijana hao kutoka vyuo na maeneo mbalimbali nchini Denmark kupitia kikundi chao cha Global Story Tellers, wanatembelea miradi yote Tanzania inayofadhiliwa na Shirika la kidini la Danmission, na kwa Wilaya ya Korogwe, taasisi hiyo kupitia Shirika la Uhifadhi wa Misitu ya Asili Tanzania (TFCG), inafadhili Mradi wa Tunza Uumbaji (Care for Creation). Mradi huo kwa Wilaya ya Korogwe, unajishughulisha na uhifadhi wa misitu ya asili na mazingira.kwa kuwawezesha wananchi kiuchumi kwa kuwapa elimu ya kilimo cha mbogamboga, maharage, mahindi, ufugaji wa nyuki, kuwapa vifaa kwa ajili ya ulinz...