SHERIA 9 KUWABANA WASANII NA WATOA MAUDHUI MTANDAONI.

  Timothy Marko DmNewsOnline 

             DAR ES SALAAM.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi Patrobas Katambi amewataka Wasanii mbalimbali wa Bongo flavour na Watengeza maudhui Mtandaoni Kujiepusha na mikingano ya Sheria (9)za mitandaoni ikiwemo kutoa Lugha Chafu mitandaoni.

Akizungumza Leo  September 2, 2026 Waziri Katambi amesema kuwa sheria  zingine  ambazo zimetajwa nipamoja na sheria ya makosa ya kutukana nakutoa Lugha Chafu za matusi na kudhalilisha  ya 89(1)a Mitandaoni adhabu yake nikifungo cha mwaka mmoja jela.

"Sheria zingine nipamoja sheria ya makosa ya kupigana pamoja na mashambulio katika Eneo la Umma(affray) S.87ambapo kifungo chamiezi 6 au faini hadi Shilingi 1000,00, Vitisho vya  kumdhuru au kumpiga mtu S.89(2)"Amesema Waziri wa Mambo ya Ndani Patrobas Katambi. 

Waziri wa Mambo ya Ndani Katambi Ameongeza kuwa kuonesha kitendo kisicho cha maadili uchafu hadharani S.176(f) Faini Shilingi 1000,00  kifungo hadi miezi mitatu  au vyote.

Amesisitiza kuwa Sheria zingine nipamoja na kujitangaza  au kushawishi kwa madhumuni ya Uasherati S.176(g) Faini hadi Shilingi 1000,00  au kifungo cha miezi mitatu.

"Uasherati Prostution hadharanj S.176 (a)faini Shilingi 1000,00 kifungo miezi mitatu  au vyote "Amebainisha Katambi. 

Sheria Nyinginezo nipamoja Maonesho Machafu yanayopotosha Maadili S.175 kifungo cha miaka miwili au faini 200,000,  Ushoga kati ya wanaume S.157 kifungo cha miaka mitano jela, Kuvunjia  mwanamke heshima kwa maneno au ishara jela miaka 5 faini Shilingi 200,000 au vyote.

Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

MWAKIPOSA ASHINDA NAFASI YA UWENYEKITI WA WENYEVITI WA SERIKALI YA MTAA MKOA WA DAR ES SALAAM

KILINDI BARABARA BADO NI CHANGAMOTO