Posts

Showing posts from August, 2026

FIBERHOME YAUNGA MKONO JITIHADA ZA SERIKALI KUBORESHA MAWASILIANO.

Image
  Na Mwandishi wetu,DmNewsonline                     WAZIRI  wa Mawasilano na Teknolojia ya Habari Angellah Kairuki alizindua awamu ya pili ya Mradi wa "Fiber mlangoni kwako"unaotekelezwa na Shirika la Mawasiliano Tanzania(TTCL)ikiwa lengo ni kuongezea upatikanaji wa intaneti yenye kasi,bora na uhakika. Aidha Kairuki amesema mradi huo ni sehemu ya jitihada za Serikali za kuimarisha uchumi wa kidigitali kwa kuwa intaneti ya kasi inawezesha wananchi kupata fursa za elimu,ajira, biashara,ubunifu na huduma mbalimbali za kijamii na kiuchumi. Hivyo wadau wa Sekta ya Teknolojia ambao ni Kampuni ya mawasiliano ya FiberHome kutoka Nchini China imeunga mkono juhudi za Serikali kwa kueendesha kongamano (workshop)nchini Tanzania lililofanyika jijini Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya ziara yao ya kuitangaza teknolojia yao Duniani na barani Afrika (World Tour). Ziara hiyo imelenga kuleta mapinduzi makubwa ya Teknolojia ya mawasiliano na akili...

MWENYEKITI WA MTAA KOROGWE TC AONGOZA WANANCHI KUPATA CHANJO

Image
Muhudumu wa afya akitoa chanjo kwa mmoja ya watoto wa Mtaa wa Kitifu, Kata ya Mgombezi. Na Yusuph Mussa,DmNewsonline                  KOROGWE  MWENYEKITI wa Mtaa wa Kitifu, Kata ya Mgombezi, Halmashauri ya Mji Korogwe mkoani Tanga, Juma Gada, amewaongoza wananchi wake kupata Chanjo ya Polio kwa watoto chini ya miaka 10. Zoezi hilo ambalo linafanyika nchi nzima, Agosti 28, 2026 limeingia siku yake ya pili, ambapo wataalamu wa afya na wadau wengine walikuwa wanaendelea na zoezi hilo kwenye kata na mitaa ya Halmashauri ya Mji Korogwe. Gada alisema yeye kama Mwenyekiti wa Mtaa wa Kitifu ana wajibu kuona wataalamu wa afya wanapata ushirikiano kwenye zoezi hilo la chanjo ya polio, kwani ni jitihada za Serikali kuona watoto hawapati madhara, sio kwa ugonjwa wa polio tu, bali na magonjwa mengine ili kulinda afya na makuzi yao. "Nashukuru wananchi wangu wamelipokea zoezi la chanjo ya polio vizuri, na jana (Agosti 27) tulikuwa pale shule ya msingi...

JESHI LA POLISI LA WASHIKILIA 11 KWA TUHUMA ZA HUJUMA MIUNDOMBINU YA TTCL.

Image
 Na Timothy Marko, DmNewsOnline          DAR ES SALAAM JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata watu 11 wanaodaiwa kujihusisha na wizi, uharibifu, usafirishaji na biashara haramu ya miundombinu ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL).  Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Jumanne Muliro, amesema operesheni hiyo imefanyika kwa kushirikiana na kitengo cha usalama cha TTCL. Amesema hatua hiyo imechukuliwa baada ya kubainika kuongezeka kwa matukio ya wizi na hujuma dhidi ya miundombinu ya mawasiliano. Kwa mujibu wa polisi, baadhi ya watuhumiwa hukata au kuiba nyaya na vifaa vya mawasiliano, huku wengine wakihusika kuvipokea, kuvisafirisha na kuviuza. Polisi imesema baadhi ya wahalifu hulenga zaidi nyaya zenye shaba, ambayo ina thamani kibiashara.  Hata hivyo, imesisitiza kuwa wizi wa vifaa hivyo unasababisha madhara makubwa kwa wananchi na taasisi zinazotegemea huduma za mawasiliano.  SACP Muliro amesema uhalifu huo ...

DC KOROGWE: ZOEZI LA CHANJO YA POLIO LIUNGWE MKONO

Image
Mhudumu wa afya Zahanati ya Kitifu akitoa chanjo kwa mtoto mchanga. Na Yusuph Mussa, DmNewsonline                      KOROGWE  MKUU wa Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga William Mwakilema amewataka wazazi, walimu, jamii na wananchi kutoa ushirikiano ili kukamilisha zoezi la utoaji chanjo ya matone kwa watoto wenye umri chini ya miaka 10. Akizungumza leo Agosti 27, 2026 kwenye Uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Chanjo ya Polio Awamu ya Kwanza, Halmashauri ya Mji Korogwe, uliofanyika Shule ya Msingi Mtonga, alisema chanjo hiyo ni muhimu kwa watoto kwa ajili ya kujikinga na maradhi. "Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Mpango wa Taifa wa Chanjo inaendelea kutekeleza kampeni hii kwa lengo la kuwakinga watoto wenye umri chini ya miaka 10 dhidi ya ugonjwa wa polio, ambao unaweza kusababisha kupooza na ulemavu wa kudumu. Chanjo itatolewa kupitia shuleni, vituo vya kutolea huduma za afya na nyumba kwa nyumba, ili kuhakikis...

DKT.NCHIMBI:NITAENDELEA KUWA RAIA MWEMA.

Image
 Na Mwandishi wetu, DmNewsOnline  MAKAMU  wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Balozi Dkt.EmmanuelJohn Nchimbi amejiuzulu Leo.  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ofisi ya Makamu wa Rais mjini Dodoma  ili eleza kuwa Dkt. Nchimbi amejiuzulu kwa mujibu wa ibara 50(2)C pamoja na 149(2) ya katiba ya Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania.  Katika Barua yake aliyomwandikia Rais, Agosti 28,2026 Dkt.Nchimbi amesema kuwa mnamo Agosti 27 Mwaka jana alimwaidi kushirikiana  na Rais Wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa uwezo wake na kwa Uaminifu mkubwa nakusisitiza kuwa  ataachia ngazi siku yoyote. "Nitaachia nafasi hii nimejiridhisha kuwa Mheshimiwa Rais pasipo shaka anahitaji mabadiliko kwa hiyo nimetimiza Ahadi yangu" Amesema Dkt.Emanuel Nchimbi.  Dkt..Nchimbi katika Barua yake aliyomwandikia Rais alieleza kuwa amekishukuru Chama chake kwa imani waliyonayo kwake nakusisitiza kuwa ataendelea kuwa Raia mwema Watanzania.

ZANZIBAR YAPEWA FURSA YA KUWA MWENYEJI WA TUZO ZA 33 ZA WORLD TRAVEL AWARDS

Image
Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline           DAR ES SAAM ZANZIBARA imepewa fursa ya kuwa mwenyeji wa Tuzo za 33 za World Travel Awards, hatua inayolenga kuongeza utambulisho wa visiwa hivyo katika ramani ya utalii duniani na kufungua zaidi fursa za uwekezaji katika sekta hiyo. Zanzibar inatarajia kupokea zaidi ya wageni 250 kutoka mataifa mbalimbali watakaoshiriki katika hafla hiyo, wakiwemo wawekezaji katika sekta ya hoteli pamoja na wawakilishi wa mashirika ya ndege. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Agosti 24, 2026, Mwenyekiti wa Bodi ya Kamisheni ya Utalii Zanzibar, Suleiman Ali Mohamed, amesema kuwa kuwa mwenyeji wa tuzo hizo ni fursa kubwa kwa Zanzibar kutangaza vivutio vyake vya utalii, kukuza uwekezaji na kuhakikisha wananchi wananufaika na sekta hiyo kupitia dhana ya utalii endelevu. Amesema Serikali inaendelea kuimarisha miundombinu ya utalii ili kuwezesha sekta hiyo kukua zaidi na kuongeza mchango wake katika uchumi wa Zanzibar...

DKT. BASHIRU AFUNGUA KONGAMANO LA NNE LA KIMATAIFA LA UVUVI NA UKUZAJI VIUMBE MAJI

Image
  Timothy  Marko, DmNews online             DAR ES SALAAM.  WAZIRI  wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. BashirAlly Kakurwa, leo Agosti 24, 2026 amefungua Kongamano la Nne la Uvuvi na Ukuzaji Viumbemaji (4tFAR4ViBE) linalowakutanisha Wanasayansi, watafiti na wadau wa uvuvi na wakuzaji viumbe maji na wataalam wa vyuo vikuu kutoka katika Nchi 17 ikiwemo mwenyeji Tanzania kujadili kuhusu maendeleo endelevu ya sekta ya uvuvi na ukuzaji viumbe maji na kuweka wazi kiwa sekta ya uvuvi zinahitaji sayansi na tafiti ili kuwanufaisha wavuvi. Kongamano hilo linalofanyika kwa siku tatu katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere International Convetion Center (JNICC) Mhe. Balozi Dkt. Bashiru amewasisitiza wataalam hao kutumia kongamano hilo kujadili kwa kina jinsi ya kutumia sayansi na tafiti kwa ajili ya uvuvi endelevu na ukuzaji viumbe maji. "Shughuli za uvuvi ni sayansi, ni jambo linalohitaji utaalam wa wanasayansi na shughuli nyeti...

SERIKALI KUTOA MAFUNZO KWA WAVUVI KUKUZA SEKTA YA UVUVI.

Image
  Timothy Marko DmNewsOnline             DAR ES SALAAM.  WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Dkt Bashiru Ali Kakurwa amesema Serikali itaendelea kuboresha Sekta ya Uvuvi wa Bahari kuu pamoja na Maziwa na kuwajengea Uwezo watalamu katika Sekta hiyo ili kuleta tija na ufanisi.  Akizungumza Leo Agosti24,2026jijini Dar es Salaam Waziri wa Mifugo na Uvuvi Bashiru Ali kakurwa amesema kuwa Kongamano la siku tatu la  kisayansi na Uvuvi lililoanza Agosti 24 hadi 27 linalenga kujadili taarifa za kiutafiti ikijumuisha vyuo vya masuala ya uvuvi sambamba nataasisi za masuala ya Uvuvi katika Ukanda wa Afrika Mashariki.  "Lengo ni kuandaa mapendekezo  juu ya utunzaji naukuzaji wa Rasmali Bahari "Amesema Waziri wa Uvuvi  Dkt.Bashiru Ali kakurwa.  Dkt.Kakurwa ameongeza kuwa kuanzia mwaka wa fedha wa Julai 2026 /2027 Serikali imelenga kuhakikisha Sekta ya Uvuvi inachangia pato la taifa.  Amesisitiza kuwa Serikali imelenga kujenga meli ...