SERIKALI KUTOA MAFUNZO KWA WAVUVI KUKUZA SEKTA YA UVUVI.
Timothy Marko DmNewsOnline
DAR ES SALAAM.
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Dkt Bashiru Ali Kakurwa amesema Serikali itaendelea kuboresha Sekta ya Uvuvi wa Bahari kuu pamoja na Maziwa na kuwajengea Uwezo watalamu katika Sekta hiyo ili kuleta tija na ufanisi.
Akizungumza Leo Agosti24,2026jijini Dar es Salaam Waziri wa Mifugo na Uvuvi Bashiru Ali kakurwa amesema kuwa Kongamano la siku tatu la kisayansi na Uvuvi lililoanza Agosti 24 hadi 27 linalenga kujadili taarifa za kiutafiti ikijumuisha vyuo vya masuala ya uvuvi sambamba nataasisi za masuala ya Uvuvi katika Ukanda wa Afrika Mashariki.
"Lengo ni kuandaa mapendekezo juu ya utunzaji naukuzaji wa Rasmali Bahari "Amesema Waziri wa Uvuvi Dkt.Bashiru Ali kakurwa.
Dkt.Kakurwa ameongeza kuwa kuanzia mwaka wa fedha wa Julai 2026 /2027 Serikali imelenga kuhakikisha Sekta ya Uvuvi inachangia pato la taifa.
Amesisitiza kuwa Serikali imelenga kujenga meli tatu za Uvuvi ilikuweza kukuza Uvuvi wa Bahari kuu.
"Tunatajia kujenga meli nne mbili zitajengwa Tanzania bara mbili Tanzania visiwani" Amesema Waziri wa Mifugona Uvuvi Dkt.Bashiru kakurwa.
Aidha kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi (TAFIRI) Ismael Kimerei amesema Kongamano hilo linalenga kujadili taarifa za kiutafiti ikijumuisha vyuo na taasisi za ufiti.
Amesema Agenda nyingine nipamoja na kujadili Rasmali Bahari ilikuweza kuchangia pato la taifa na kustawisha uchumi.
"Sambamba nahayo Tunalenga Uzalishaji wa Uzalishaji bora wa Chakula cha Samaki,kuzalisha vifaranga bora vya Samaki lengo kufikia tani 600,000"Mkurugenzi wa taasisi ya Utafiti Tafiri Ismael Kimerei. 






Comments
Post a Comment