MBUNGE LUTEVELE :MARUFUKU WALIMU KUFANYA BIASHARA ZA KACHORI DARASANI

  Na Mwandishi wetu,DmNewsonline

               IRINGA _MAFINGA 


Mbunge wa Jimbo la Mafinga Dickson Lutevele (Villa), amepiga marufuku walimu kujihusisha na biashara ndogondogo darasani na kulazimisha wanafunzi kununua bidhaa hizo

Hatua hiyo imekuja kufuatia malalamiko ya baadhi ya  wazazi wa mtaa wa Lutalawe kata ya Changarawe, waliodai kuwa baadhi ya walimu wamekuwa wakiendesha biashara ndani ya maeneo ya shule    hali inayosababisha kero kwa wazazi ya kutoa fedha kwa Watoto kila siku.

Walimetaka mbunge kuingilia kati suala hilo ili kupunguza mzigo wa kifedha kwa familia kwani wanalazimika kutoa fedha kiasi cha shilingi 200 hadi 500 kila siku ili mtoto akanunue kachori kwa mwalimu, 

Akijibu malalamiko hayo, mh. Lutevele alitoa agizo kwa maafisa elimu na watendaji kuhakikisha wanakomesha mara moja vitendo hivyo nakueleza kuwa serikali tayari imepiga marufuku michango holela mashuleni, hivyo walimu wanaolazimisha wanafunzi kununua bidhaa zao wanafanya kitendo kinachofanana na mchango usio halali.

Afisa elimu wa kata ya Changarawe Shaban Nyigo ameahidi kulifanyia kazi suala hilo mara moja huku akibainisha kuwa walimu hawaruhusiwi kufanya biashara shuleni na yeyote atakayebainika atachukuliwa hatua kwa mujibu wa taratibu za kazi.

Mbunge Dickson Lutevele amehitimisha ziara ya siku tatu jimboni kwake, ambapo alipata fursa ya kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi kwa kushirikiana na wataalamu kutoka katika halmashauri yam ji Mafinga na wilaya ya Mufindi.


Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

DKT. KIJAZI KUSIMAMIA MIRADI YA MAENDELEO JIMBO LA KOROGWE MJINI.