TRA :TUNAWEKEZA MIFUMO YA KIGITALI KUONGEZA WIGO WALIPA KODI.

  Timothy Marko,DmNewsOnline 

           DAR ES SALAAM. 

MAMLAKA ya Mapato Nchini Tanzania (TRA) imesema ili kuweza kuendana na kasi ya mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia taasisi hiyo imelenga kutoa huduma zake kwa njia ya Kidijitali ili kuzifikia biashara kirahisi zaidi.

Akizungumza Leo April 29,2026 jijini Dar es Salaam Kamishina wa Mamlaka ya Mapato Nchini CPA Yussufu Mwenda amesema kuwa biashara nyngi siku hizi zinahifadhiwa kwenye Maghala na kuuzwa kwa njia za kimtandao.

"SaSa hivi kuna makundi ya walipa kodi kwa njia ya Kidijitali, wengi wao hawalipi kodi tunahitaji Usimamizi wa biashara za mitandaoni ,nilazima tuje na mawazo bunifu "Amesema Kamishina Mwenda. 
.
Mwenda Ameongeza kuwa katika kutafuta mawazo bunifu taasisi hiyo ili weza kupata mawazo bunifu takriban 1,5581  ambapo kati ya hayo 600 yaliweza kushinda kwa kushirikiana na Wananchi.

Amesisitiza kuwa katika kutafuta mawazo bunifu yatakayo chochea mabadiliko ya kodi na ukuaji wa biashara Nchini, zawadi zitatolewa kwa atakaye kuja na mawazo bunifu yatakayo chochea Mawazo ambapo katika Awamu ya kwanza washiriki 106 waliweza kupita

"Katika awamu ya pili tunatarajia kuwapatia Shilingi 1000,00 kwa atakaye kuja na wazo bunifu lakuimarisha taasisi "Amesisitiza CPA Mwenda.

Naye Makamu wa Rais wa Chember ya Wafanyabishara Nchini Boniface Ndegeu amesema kuwa Taasisi hiyo inaiunga mkono Mamlaka hiyo ya kodi Nchini katika kukuza ufanisi wa Biashara. 
Amesema kuwa maboresho ya Mamlaka ya Mapato Nchini yatawezesha kuongeza tija katika Sekta ya biashara. 

"Mapendekezo haya yataongeza wigo walipakodi kutoka watu milioni tatu kati ya milioni sitini"Amesema Ndegeu.

Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

DKT. KIJAZI KUSIMAMIA MIRADI YA MAENDELEO JIMBO LA KOROGWE MJINI.