TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MASHINDANO YA MISS W0RLD 2027.
Timothy Marko DmNewsOnline.
DAR ES SALAAM.
TANZANIA inatarajiwa kuwa Mwenyeji wa Mashindano ya 74ya Miss World yanayotarajiwa kufanyika Mwakani2027.
Akizungumza Leo April 20,2026katika Hafla ya Utiliaji saini wa Mkataba wakuwa mwenyeji wa Mashindano hayo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Habari, Sanaa, utamaduni Paul Makonda amesemakuwa Mashindano hayo yatajumuisha Nchi Takribani 130 akiwemo mwenyeji wa mashindano hayo ambaye niTanzania.
" Zaidi ya Vituo vya TELEVISION vipatavyo 100 na watazamaji Zaidi 20,000 wanatarajiakuhudhuria Mashindanou haya"Amesema Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni Paul Makonda.
Waziri Makonda Ameongeza kuwa Mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika kwa muda wa siku ishirini nane mfululizo.
Amesisitiza Mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika Tanzania baada ya mashindo ya mwaka huu 2026 kufanyika Nchini Vietnam ambapo Msimu ujao yanatarajiwa kufanyika Nchini Tanzania.
"Tanzania itakuwa mwenyeji wa pili katika Nchi za bara Afrika baada ya Nchi Afrika kusini kuwa mwenyeji wa mashindano hayo "Amebainisha Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni Paul Makonda.
Naye Mwenyekiti wa Mashindano Miss World Miss Julia Mollel amesema kuwa kupitia Tanzania kuwa Mwenyeji wa Mashindano ya 74ya Miss World Tanzania itapatafursa kujitangaza katika sekta ya Utalii.
Amesema kupitia Miss World Tanzania itajitangaza kupitia Hotel zakitalii ambapo zaidi ya Nchi 144 zinatarajiwa kushuhudia Mashindano hayo.
"Kupitia Mashindano haya yatoa fursa ya makampuni nahoteli mbalimbali kuweza kujitangaza Duniani kote ,hii ni fursa Muhimu katika kutangaza kimataifa "Amesema Mwenyekiti wa Mashindano ya Miss World Julie Mollel.

Comments
Post a Comment