TUME YA PDPC YAKABILIWA NA CHANGAMOTO YA MABADILIKO YA AKILI UNDE

  Timothy Marko DmNewsOnline 

            DAR ES SALAAM. 

TUME ya Udhibiti wa Taarifa Binafsi Nchini imesema moja ya Changamoto inayoikabili Taasisi hiyo niukuaji wa Teknolojia ya Akili unde(AI) bila kuzuia Maendeleo ya kiuchumi wa Kidijitali. 

Akizungumza Leo  June 29,2026jijini Dar es Salaam kwenye Kongamano la kwanza la Ulinzi wa taarifa Binafsi Nchini Tanzania(1st Tanzania Annual Data Privacy Conference )Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nchini Dk.Switbetrt Mkama amesema kuwa Taarifa Binafsi ni Utambulisho wa mtu hivyo haina budi kulindwa,Taasisi zina umuhimu wa kuzilinda Taarifa hizo katika kuelekea Uchumi wa kigitali. 

"Mamlaka ya Ulinzi wa taarifa Binafsi zinawajibu kushirikiana na Taasisi za kikanda Barani Afrika katika Ulinzi wa taarifa Binafsi katika kuelekea Uchumi wa kigitali "Amesema Naibu Waziri Dkt Mkama.

Dkt.Mkama Ameongeza kuwa katika kuelekea Uchumi wa kigitali suala la Faragha Nimuhimu ilikuweza kufikia Dira ya Maendeleo ya 2050.

"Serikali imetunga sheria ya Ulinzi wa taarifa Binafsi 2022 katika kuwasajili wachakataji wa taarifa Binafsi "Amesisitiza Dkt.Mkama.

Naye Mkurugenzi wa Tume ya Ulinzi  wa taarifa Binafsi Dk.Adard Rajabu amesema kuwa Mchakato wa Ulinzi wa taarifa Binafsi unakabiliwa na Changamoto ya Mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia, Hali iliyobadili mfumo wakuishi.

Dkt.Rajab amesema Taasisi zinaumuhimu wa kipekee katika kulinda taarifa Binafsi kuelekea Uchumi wa Kidijitali .
"Mamlaka  ya Ulinzi wa taarifa Binafsi Nilazima zikuze ushirikiano nataasisi nyinginenezo katika kuimarisha Ulinzi wa taarifa Binafsi "Amebainisha Dkt.Rajab.

Aidha,kwa upande wake Mkurugenzi wa Tume ya Ulinzi wa taarifa  Binafsi Nchini Dkt.Emanuel Mkila amesema Hivi Karibuni Tanzania imeshuhudia matumizi ya Mtandao lakini kumekuwa na Changamoto ya kukabiliana Ulinzi wa taarifa Binafsi. 

Amesema Tume hiyo iliyoanzishwa mwaka 2022imendelea kutoa Elimu ya Haki ya Faragha. 

"Pia tumeimendelea kuwajengea Uwezowamaafisa wa Tume ya Ulinzi wa taarifa Binafsi, "Amesema Dkt. Mkila.

Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

MWAKIPOSA ASHINDA NAFASI YA UWENYEKITI WA WENYEVITI WA SERIKALI YA MTAA MKOA WA DAR ES SALAAM

DKT. KIJAZI KUSIMAMIA MIRADI YA MAENDELEO JIMBO LA KOROGWE MJINI.