TRA YAJITOSA KUSAIDIA JAMII

 Na Eliasa Ally DmNewsonline

          IRINGA 

MAMLAKA  ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Iringa  imeendelea kuonyesha mshikamano na jamii kwa kuwasaidia wagonjwa wasio na uwezo wa kulipia gharama za matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa.

Zoezi hilo limefanyika Juni 25, 2026, ikiwa ni sehemu ya shughuli zinazoendelea kuelekea maadhimisho ya miaka 30 tangu kuanzishwa kwa TRA.

Mkurugenzi wa idara ya fedha kutoka TRA Dinah Msuya amesema TRA wamekabidhi misaada mbalimbali ikiwemo malipo ya baadhi ya bili za matibabu kwa wagonjwa wenye uhitaji, pamoja na zawadi kwa wagonjwa na wauguzi wanaotoa huduma hospitalini hapo.

Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa, Dkt. Alfred Mwakalebela, ameipongeza TRA kwa hatua hiyo na kutoa wito kwa taasisi nyingine za umma na binafsi kuiga mfano huo kwa kuwasaidia wananchi wenye mahitaji mbalimbali, hususan katika sekta ya afya.

Nae mmoja wa wagonjwa walionufaika na msaada huo ameishukuru TRA kwa moyo wa kujitoa na kuwajali wananchi wenye changamoto za kifedha, akisema msaada huo umewapa matumaini na kupunguza mzigo mkubwa waliokuwa nao.   

Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

MWAKIPOSA ASHINDA NAFASI YA UWENYEKITI WA WENYEVITI WA SERIKALI YA MTAA MKOA WA DAR ES SALAAM

DKT. KIJAZI KUSIMAMIA MIRADI YA MAENDELEO JIMBO LA KOROGWE MJINI.