WAMILIKI WAMASHAMBA SOMELO_ ZINGIZIWA WAJA JUU WASEMA KUNA MTU ANATAKA KUPORA MAENEO YAO ,WATISHIA KWENDA MAHAKAMI.
Na Mwandishi wetu,DmNewsonline
DAR ES SALAAM
WAMILIKI wa shamba lenye heka 90 Iililoko Mtaa wa Somelo, Kata ya Zingiziwa Ilala,jijini Dar es Salaam, wamelalamikia kuwapo kwa mtu aliyetajwa Obadia Mkwabi anayevamia maeneo na kutaka kuyakatakata vipande kwa lengo la kuuza viwanja.
Wamesema kuwa mtu huyo alikuwa anachukua hatua hiyo akidhani kwamba maeneo hayo hayana wamiliki lakini licha ya kupewa taarifa kwamba maeneo hayo yanawenyewe bado aliendelea kuwa mkaidi hivyo wamepanga kumfikisha Mahakamini endapo ataendelea na kusudio lake lakutaka kupora.
Wakizungumza Mei 2, mwaka huu, mbele ya waandishi wa habari waliofika shambami hapo mmoja wa wamiliki wa shamba hilo, Alfonce Mallya, amesema mtu huyo anashirikiana na baadhi ya viongozi waliopewa mamlaka ya kuongoza wananchi kutaka kuwadhulumu haki ya wengine
Akizungumzia shamba hilo Mallya amesema alinunua mwaka 1990, akiwa hajastaafu katika utumishi wa umma kwa kushirikiana na mstaafu mwezake
Amesema baada ya kununua shamba hilo na jirani yake huyo , Florian Bubelwa, wanashangaa kuona Mapema mwezi huu mvamizi huyo ameonekana akiwa shambani hapo na kupima shamba lao kwa lengo kujua ukubwa wake na baadae akate viwanja.
Mallya kuchelewa kuendeleza shamba hilo kulitokana na yeye kupata maradhi na mwaka 2001 kwenda India kutibiwa ambapo alikaa kwa muda mrefu bila kufika shambani kwake na mvamizi huyo alitumia fursa hiyo kutaka kujimilikisha shamba hilo.
Mallya amesema mvamizi huyo anashirikiana na baadhi ya viongozi wa kisiasa kutaka kupora mali yao kinyume cha utaratibu wa kisheria
Naye, Florian Bubelwa, ambaye ni mmoja wa mmiliki wa shamba hilo, amesema kwaupande wake alinunua sehemu ya ardhi hiyo mwaka 1988 kabla ya kustaafu katika utumishi wa umma
Bubelwa amesema anavyo vielelezo vyote vinavyoonesha uhalali wa kumiliki shamba hilo.
Amesema kutokana na kuwapo kwa tukio hilo anakusudia kwenda mahakamani ili haki iweze kutendeka kwani tayari ameshawaandaa wanasheria wake kwa ajili ya kuendesha kesi hiyo
Bubelwa amesema akiwa mmiliki halali wa shamba hilo, ataendelea kulihudumia na kama kuna mtu anadai la kwake atathibitisha kwa vielelezo mahakamani.
"Tayari nimeshawasiliana na wanasheria wangu ili jambo hili liende Mahakamini "amesema Bubelwa.
Kwa upande wa ofisi ya Serikali ya mtaa wa somelo chini ya mwenyekiti Hassan Rashi alipotafutwa kwa njia ya simu ili kujibu malalamiko ya watu wake amejibu kuwa kuhusu shamba hilo amepata malalamiko kutoka kwa wananchi .
Ameongeza kuwa licha ya kupata malalamiko hayo lakini hajuwi mmiliki wa mashamba hayo nani kwa maana hawajawahi kufika ofisini kwake kwa ajili ya Kuzungumzia jambo hili .
Hata hivyo aliwataka waandishi wasitoke wamsubiri ili aje kutoa ufafanuzi zaidi lakini hadi waandishi wanaondoka eneo la tukio mwenyekiti huyo alikuwa bado hajafika na simu yake ilikuwa haipatikani tena.

Comments
Post a Comment