SERIKALI KUTOA ML.50 KWA KINARA SHINDANO LA VIJANA UCHUMI CHALLENGE 2026

   Na Mwandishi wetu,DmNewsonline

                PWANI 
 
SERIKALI  imekuja na mpango kabambe  wa kuanzisha shindano  linalojulikana kwa jina la Vijana uchumi Challenge lenye lengo la kuwakutanisha vijana mbali mbali ili kutoa mawazo  yenye kuleta tija katika kuisaidia Serikali katika nyanja tofauti  ikiwemo uchumi na maendeleo.

Hayo yamebainishwa na  Naibu Katibu  Ofisi ya Rais maendeleo ya vijana Dkt.  Kedmon Mapana  wakati wa halfa ya uzinduzi rasmi wa kambi maalumu  kwa ajili ya usahili wa vijana wapatao 100 bora  ambao wamepata fursa ya kuchaguliwa kati ya vijana elfu 7852 walioshiriki hapo awali kutoka mikoa  27 ya Tanzania bara na visiwani.

Pia amebainisha kwamba ana imani vijana hao  100 ambao wamechaguliwa na kuweka kambi wataweza kuleta matokeo chanya na kwamba serikali itaendelea kushirikiana nao bega kwa bega na kuchukua mawazo yao ambayo watakwenda kuyafanyia kazi na kuyaendeleza katika maeneo mbali mbali.

"Sisi kama serikali tumeona ni muhimu sana kuwashirikisha vijana wetu wa Tanzania ambao ndio Taifa letu la kesho katika shindano hili ili waweze na wao kuchangia mawazo yao mbali mbali ambayo  yataweza kuketa tija zaidi katika kuisaidia serikali katika nyanja mbali mbali za kiuchumi na mambo mengine ya  kimaendeleo na mimi nashukuiru sana vijana hao 100 kwa kujitokeza kwa wingi,"amesema Naibu Katibu huyo.
 
Kadhalika amesema   baada ya kambi hiyo ya vijana watachaguliwa kutoka 100 hadi kufikia vijana 10 ambao watakwenda katika shindano la fainali litakalofanyika mwezi ujao tarehe 6 na kwamba mshindi wa kwamba atajinyakulia sh.milioni 50, mshindi wa pili milioni 30 na mshindi wa tatu  milioni 20 na wengine waliobaki watapewa kifuta jasho

 Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya Kitaifa ya shindano hilo la vijana Uchumi Challenge Joseph Malekele amesema kwamba washirki hao  wataweka kambi kwa kipindi cha muda wa siku nne katika  katika  shule ya Uongozi Mwalimu Julias Nyerere iliyopo  Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani ambapo pia watapatiwa mafunzo kutoka kwa jopo la majaji mbali mbali.

Mwenyekiti huyo amesema lengo kubwa la  kuandaa shindano hilo ni kuweza kupata mawazo bunifu kutoka kwa vijana ambayo yanaweza kutekelezeka na kuchangia kwa kiasi kikubwa  masuala mazima ya kukuza  uchumi pamoja na kuweka misingi endelevu katika maendeleo katika sekta mbali mbali za kilimo, usafirishaji, biashara na mambo mengineyo.
 
Nao baadhi wa vijana hao ambao wamepata fursa ya kuingia katika kambi hiyo akiwemo Raiani Amour na Adrian Thomas wamebainisha kwamba wana imani mawazo na ubunifu wao utaweza kwenda kuleta matokeo chanyaa katika kuwasaidia vijana hasa ambao wamekuwa na changamoto katika ukosefu wa ajira.

Aidha wameipongeza kwa dhati serikali ya awamu ya sita kwa kushirikiana na Wizara ya vijana kwa kuweza kuona umuhimu mkubwa wa kuwakutanisha vijana kutoka maeneo mbali mbali kwa ajili ya  kutoa mawazo yao mbali mbali ili kuweza kuisaidia serikali katika mambo mbali mbali.

Kilele cha Shindano hilo  la Vijana Challenge kwa mwaka 2026 linatarajiwa kufanyika  Julai   6 mwaka huu Jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan
                             

Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

MWAKIPOSA ASHINDA NAFASI YA UWENYEKITI WA WENYEVITI WA SERIKALI YA MTAA MKOA WA DAR ES SALAAM

DKT. KIJAZI KUSIMAMIA MIRADI YA MAENDELEO JIMBO LA KOROGWE MJINI.