DEOGRATIUS NDEJEMBI KUTOWAVUMILIA WACHELEWESHAJI WA MIRADI VIJIJINI.
Timothy Marko DmNewsOnline
DAR ES SALAAM
WAZIRI wa Nishati Deogratius Ndejembi amesema Serikali Hatowavumilia Wakandarasi Wazawa watakaochelewesha Miradi ya Umeme kwa wakati ,Na baadala yake watanyang'anywa Zabuni hiyo nakutopewa tena katika Miradi hiyo.
Akizungumza Leo juni 22,2026 jijini Dar es Salaam Waziri Ndejembi amesema kuwa Serikali imelenga kuimarisha upatikanaji wa umeme katika maeneo ya vijijini ili kuweza kuchochea Shughuli za Kiuchumi.
"Umeme ni hitaji muhimu kama ilivyo mahitaji Mengine,Siku hizi Umeme sio anasa bali nikichocheo kizuri cha Kiuchumi "Amesema Waziri Ndejembi.
Ndejembi Ameongeza kuwa Umeme ni Nyenzo Muhimu katika kuimarisha sekta ya Elimu na kukuza Mazingira ya kujifunza kwa Wanafunzi mashuleni,nakukuza Shughuli za kiuchumi.
Amesisitiza kuwa katika Dira ya Maendeleo 2050 Umeme ndio Nyenzo Muhimu katika Utekelezaji wa Dira ya Maendeleo hususan katika Maendeleo ya Viwanda na sekta Kilimo.
"Dira ya Maendeleo 2050 imelenga kuzalisha Umeme kutoka megawatts 1500 hadi megawatts 4000 ,2050"Amesisitiza Ndejembi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Nishati Vijini (REA) Balozi Meja Jenerali Mstaafu Jacob Kingu amesema kuwa Bodi hiyo itawapatia tunzo Wakandarasi wazawa watakaofanya Vizuri ,ilikuhakikishaVitongoji vyote Nchini vinafikiwa na Huduma ya Umeme.
Amesema Taasisi hiyo inaandaa kanzi Data ya Wakandarasi wa Ndani wanaotekeleza miradi kwa wakati nakuwatafutia Masoko nafursa katika nje ya Nchi.
"Bodi itaendelea kushirikiana na Menejimenti katika kutekeleza Miradi kwa wakati"Amesema Mkurugenzi wa Bodi ya REA Meja Jenerali Jacob kingu.
Aidha,kwa upande Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijini (REA)Mhandisi Hassan Said amesema Taasisi hiyo ina miradi ya Gesi ya kupikia na Mafuta.
Amesema Takribani Miradi 32 imemeweza kukamilika kabla ya wakati.










Comments
Post a Comment