JESHI LA POLISI KUENDELEA NA UCHUNGUZI MAUAJI MBEZI.

   Timothy Marko, DmNewsonline

       DAR  ES SALAAM. 


JESHI la polisi Kanda Maalumu ya Dar es  Salaam limesema linaendelea na Uchunguzi wa kina juu ya Ramadhan Jafarry Muno (47) Baada kudaiwa kupotea huko  Mbezi Wilaya ya Ubungo akiwa kwenye  Nyumba yake. 

Akizungumza Leo juni 23,2026 jijini Dar es Salaam Kamishna wa Polisi  Kanda Maalumu ya Dar  es Salaam ( CP) Jumanne Murilo  amesema kuwa tukio hilo lili tokea juni 16,mwaka huu huko Mbezi Kimara Wilayani  Ubungo, Baada ya Jeshi hilo kutarifiwa kuwa mtu huyo amepotea katika Mazingira ya kutatanisha.

"Katika Uchunguzi wa awali Jeshi la polisi  tulibaini kuwa aliye fanya tukio hilo ni Mtoto wa Marehemu huyo Juma Ramadhani(21) Ambapo alieleza kuwa Amemuuwa Baba yake" Amesema Kamanda Murillo. 

Murilo Ameongeza kuwa Jeshi hilo linaendelea na Uchunguzi wa mtoto huyo kubaini chanzo halisi cha kumua Baba yake.

Amesisitiza Baada ya Uchunguzi wa  tukio hilo hatua kali zitachukuliwa juu ya Mtuhumiwa huyo. 

Katika Hatua nyingine Kamishna Murillo Amesema waendelea kufanya Uchunguzi wa  taarifa zisizo rasmi kuwa kuna Baadhi ya watu wanataka kuandamana Julai 7 Mwaka huu na kusisitiza kuwa jeshi hilo linachunguza juu ya tukio hilo linalodaiwa kutajwa na Baadhi ya Wanaharakati.

 Amebainisha kuwa linafanyia kazi juu ya mipango hiyo kwa weledi kabla ya kuwakamata Watuhumiwa wanaotaka kufanya maandamano hayo.
Amesema  Suala la Upelelezi linahitaji Utulivu ,ushaidi unaokubalika Mahakamani. 

"Hata suala la kuimarisha Ulinzi na Usalama kwenye Baadhi ya mikutano ya Kisiasa  tunafanya kwa kuzingatia Weledi "Amesisitiza Kamanda murilo

Kamanda  Murilo amewambia Waandishi wa Habari kuwa moja ya majukumu ya jeshi hilo mara baada ya kupata fununu za matukio ya Uvunjifu wa amani ni kufanya  uchunguzi,kupeleleza na kukusanya Ushaidi ili kupeleka Mahakamani juu ya mashauri.

"Msemaji wetu wa Jeshi la Polisi Afande David Misime ameshasema juu ya msimamo wetu wa Julai 7 ,Mwaka huu sisi tumejipanga kuimarisha Usalama Amebainisha Kamanda Murilo.

Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

MWAKIPOSA ASHINDA NAFASI YA UWENYEKITI WA WENYEVITI WA SERIKALI YA MTAA MKOA WA DAR ES SALAAM

DKT. KIJAZI KUSIMAMIA MIRADI YA MAENDELEO JIMBO LA KOROGWE MJINI.