CHAUMA YAITAKA SERIKALI KUTENGENEZA MIFUMO WEZESHI KWA VIJANA KUJIKWAMUA KIUCHUMI.
Timothy Marko DmNewsOnline
DAR ES SALAAM.
CHAMA cha Ukombozi wa umma (CHAUMA) kimeitaka Serikali kuwatengenezea Mazingira mazuri kundi la Vijana ya kiuchumi ili waweze kujikwamua na kuondokana na tatizo la Ukosefu wa ajira Nchini.
Akizungumza juni 24,2026 jijini Dar es Salaam Mratibu wa jukwaa la Vijana wa Chama hicho (JUVICHA)Masoud Mambo amesema Vijana takriban 20,000,000 wanakabiliwa na tatizo la Ukosefu wa Ajira huku 800,000 ndio wapo katika ajira isiyorasmi
"Licha ya kuwepo kwa Mikopo kwa Vijana ,BodaBoda haiwezi kuwa mbadala wa ajira kwa Vijana Amesema Mambo.
Mambo Ameongeza kuwa Pamoja na Serikali kutenga takribani Shilingi trioni 62.33 Bado maisha ya Maafisa Usafirishaji (BodaBoda) wanaishi maisha magumu nakwamba Chama hicho kitaendelea kusimamia Ajenda za Wananchi hususa Vijana.
"Katika Mkutano wa kimataifa wa vijana wa Umoja wa Mataifa uliofanyika mwaka 1991 ,ulianisha Changamoto za kiuchumi na kisiasa zinazo wakabili vijana Amebainisha Masoud.

Comments
Post a Comment