FILAMU YA KIKULACHO KUONESHWA KUPITIA YOUTUBE KUANZIA SASA.

 Timothy Marko DmNewsonline

     DAR ES SALAAM. 

MSANII wa Bongofleva Barnaba Elias (Barnaba Class) amesema kuwa uzoefu wake katika soko la Filamu Nchini ulianza kabla ya kuanza mziki wa bongofleva nakusisitiza kuwa tasnia hiyo kwake siyo jambo jipya.

Amesema hayo leo Juni 24,2026 jijini Dar es salaam wakati wa kutambulisha seasoni ya 1 ya Kikulacho ambayo imeandaliwa na Kampuni ya Hightable Film nakwamba itakua inaomeshwa kupitia mtandao ya YouTube kwanza sasa.

"Nimeamua kuipeleka Filamu hii kwenye YouTube ninaamini kuwa itapata wataamaji wengi ikilinganishwa na kwenye Tv kwasababu baadhi ya Watazamaji hawana visimbuzi vinavyoonesha Filamu,hii inasababisha baadhi ya Watazamaji kukosa uhondo" amesema Barnaba 

Nakuongeza kuwa"Filamu hii nimeigiza katika viwango vya hali ya juu ikilinganishwa na Filamu za kutoka Nigeria na Afrika Kusini,hivyo watazamaji watafurahia kutazama Filamu ya Kikulacho".

Aidha amesema kuwa amefurahishwa na msanii mwenzake  Gabo Zegambwa kwa kimtia moyo kuwa anaweza kuigiza Filamu kwa kiwango Cha Kimataifa hali hiyo ikampelekea kupate nguvu ya kushiriki katika uandaaji wa Filamu ya Kikulacho.

Kwa upande wake Msanii wa Filamu hiyo Aisha Juma almaarufu kama 'Aisha Khan'amesema kuwa Filamu hiyo ina mvuto wa kipekee ambapo maudhui yake yanaweza kuangiliwa na rika lote na kusisitiza kuwa Filamu hiyo haichoshi kutazama.

"Filamu hii ya Kikulacho inaweza kutazamwa na Makundi rika yote ikiwemo wazee,vijana na watoto,kwani ina maudhui yenye mafunzo kwa jamii" amesema Aisha Khani.

Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

MWAKIPOSA ASHINDA NAFASI YA UWENYEKITI WA WENYEVITI WA SERIKALI YA MTAA MKOA WA DAR ES SALAAM

DKT. KIJAZI KUSIMAMIA MIRADI YA MAENDELEO JIMBO LA KOROGWE MJINI.