MWAKIPOSA ASHINDA NAFASI YA UWENYEKITI WA WENYEVITI WA SERIKALI YA MTAA MKOA WA DAR ES SALAAM
Na Angelina Mganga -DmNewsOnline BDAR ES SALAAM UCHAGUZI wa nafasi ya Uwenyekiti na Katibu Mkuu wa Umoja wa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam umefanyika Leo Juni 20,2026,na umemalizika kwa amani na utulivu. Uchaguzi huo ulikuwa na wagombea watatu ambao wamewania nafasi hiyo ya Uwenyeviti wa Wenyeviti wa Serikali ya Mtaa Mkoa wa Dar es Salaam Wagombe wa nafasi ya Uwenyeviti ni Consolatha M.Rwiza Juma A.Mwingano na Razalous A.Mwakiposa Katika uchaguzi huo Razalous A.Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi hiyo ya Uwenyekiti huku Peppino Sudi Peppino akishinda nafasi ya Katibu. Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo,Msimamizi wa Uchaguzi Kambi Sinde amesema kuwa kura zilizopigwa ni 37 na wagombea walikuwa Consolatha M.Rwiza (11),Juma A.Mwingano (2 )na Razalous A.Mwakiposa ( 24 ) hakuna kura iliyoharibika. Razalous A.Mwakiposa ameshinda Kwa kura 24 kati ya kura 37zilizopig...