WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUTOA ELIMU JUU YA MAADILI YA UTUMISHI WA UMMA.

   
   Ti mothy Marko DmNewsOnline. 

        DAR ES SALAAM.

WAANDISHI Habari wametakiwa kuwaelimisha Watumishi wa umma Nchini juu ya Maadili yao ili kuweza kufikia Dira ya Maendeleo 2050.

Akizungumza Leo Mei 19 ,2026  katika Kongamano la Waandishi wa Habari na Wahariri wa  Vyombo vya Habari Nchini (TEF)Katibu msimamizi  wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma  Kassim Mkwawa amesema kuwa katika kukuza maadili ya Viongozi wa Umma, vyombo vya Habari vinamchango wakipekee wa kuwaelimisha Watumishi wa umma juu ya Maadili ya Utumishi wa Umma. 

"Sektarieti ya Maadili ya Utumishi wa Umma imeundwa chini ya sheria namba (14) ya mwaka 1995 ya Maadili ya Utumishi wa Umma" amesema mkwawa

 Ameongeza kuwa Taasisi hiyo imelenga kukuza Watumishi wa umma walio na weledi na Uzalendo kwa Nchi yao.

Amesisitiza kuwa hivi karibuni kumekuwa na minongo'no ya kupungua kwa Uadilifu kwa Baadhi ya Watumishi wa umma huku chanzo kikubwa kikitajwa ni  Ukosefu wa Maadili ya Utumishi wa Umma na mgongano wa kimaslahi kwa Baadhi ya Watumishi wa umma "Amesisitiza  Mkwawa. 

Naye Katibu wa Ukuzaji wa Maadili Waziri Kipacha amesema kuwa chanzo kikuu  cha uvunjifu wa Maadili ya Utumishi wa umma ni Mgongano wa kimaslahi .

"Tatizo hili la mgongano wa kimaslahi halipo kwenye sekta ya Umma pekee bali Hata sekta binafsi linalo Tatizo la mgongano wa kimaslahi "Amesema Kipacha

Aidha,Wakili wa Serikali Emma Gelani Amesema kumekuwa na Baadhi ya Watumishi wa umma kuwa Wafanyabishara wakubwa na pia kuhudumu katika Serikali.

Amesema Taasisi hiyo  inapokuwa inawaita Viongozi hao hawaziwasilishi taarifa za mali zao zote kwenye Tume hiyo na badala yake kutoa taarifa za Uongo juu ya mali hizo ambapo ni kinyume cha Sheria ya Utumishi wa Umma. 

"Tume yetu tumeshawahi kuwashilikilia Baadhi ya Watuhumiwa Umma wakijiuhusisha na Biashara ya Boda Boda "AmesemaWakili waserikali Emma Gelani.

Wakili Gelani Amesema Endapo wamemtilia shaka kiongozi juu ya Ukwasi wa kiongozi, tume hiyo inashirikiana  na Ofisi ya CAG kufanya Uchunguzi wa Mali hizo.   

Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

MWAKIPOSA ASHINDA NAFASI YA UWENYEKITI WA WENYEVITI WA SERIKALI YA MTAA MKOA WA DAR ES SALAAM

DKT. KIJAZI KUSIMAMIA MIRADI YA MAENDELEO JIMBO LA KOROGWE MJINI.