WATUHUMIWA 215 WAKAMATWA KWA MAKOSA MBALIMBALI IRINGA

   Na Eliasa Ally DmNewsonline

                  IRINGA 

JESHI  la Polisi Mkoa wa Iringa limefanikiwa kuwakamata jumla ya watuhumiwa 215 kwa makosa mbalimbali katika kipindi cha Mei 1 hadi Juni 9, 2026 na kuwafikisha Mahakamani.

 Watuhumiwa hao walikamatwa kupitia misako, doria na operesheni maalumu zilizofanyika maeneo mbalimbali ya mkoa huo huku wakikutwa na mali zinazodhaniwa kuwa za wizi zikiwemo magari, vifaa vya ujenzi, vifaa vya umeme, simu za mkononi, pikipiki pamoja na mali nyingine mbalimbali.

Aidha, Juni 9, 2026 katika eneo la Igumbilo Manispaa ya Iringa, Polisi walimkamata mfanyabiashara mmoja kutoka Tunduma pamoja na wenzake watatu kutoka Dar es Salaam wakiwa na katoni 177 za vipodozi vilivyopigwa marufuku nchini, vilivyokuwa vikisafirishwa kwa basi kutoka Zambia kuelekea Dar es Salaam.

Kwa upande wa usalama barabarani, Polisi walimkamata dereva aliyekuwa akiendesha kwa uzembe na kuhatarisha usalama wa watumiaji wa barabara, hatua iliyosababisha kuondolewa barabarani na kufungiwa leseni kwa miezi sita. 

Kwa upande mwingine, jumla ya washtakiwa 155 wamehukumiwa vifungo mbalimbali kwa makosa tofauti, yakiwemo ubakaji, kupatikana na nyara za Serikali pamoja na makosa mengine ya jinai. 

Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

MWAKIPOSA ASHINDA NAFASI YA UWENYEKITI WA WENYEVITI WA SERIKALI YA MTAA MKOA WA DAR ES SALAAM

DKT. KIJAZI KUSIMAMIA MIRADI YA MAENDELEO JIMBO LA KOROGWE MJINI.