CHALAMILA AWATAKA WATENDAJI WA SERIKALI ZA MITAA KUDHIBITI MAJENZI KWENYE MAENEO YA MABALOZI.

 
  Timothy Marko DmNewsOnline 

                DAR ES SALAAM. 

MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila Amewataka   Viongozi wa Serikali ya mtaa waliopo katika Maeneo ya Mabalozi kudhibiti kasi ya Majenzi ya Majengo,nakutaka kusitisha Vibali vya Majenzi katika Maeneo hayo.

Akizungumza leo juni 15,2026 jijini Dar es Salaam katika Kongamano lililowakutanisha Watendaji wa Serikali za Mitaa na kata Albert Chalamila Amewataka Watendaji hao kusitisha vibali  kwa wanaomiliki Bar zilizozopo kwenye makazi ya watu na kuhakikisha Bar zote jijini Dar es Salaam kuwa na Vizibiti Sauti kwenye Makazi ya watu.

'"iundwe timu Maalumu kasi ya Udhibiti Majenzi kwenye maene ya Diplomatic, Ninawaomba Ndugu wenyeviti wa Serikali za mitaa kutambua nafasi zenu"Amesema Chalamila. 

Chalamila Ameongeza kuwa nivyema Wenyeviti wa Serikali za mitaa kufunga Bar zote ambazo hazina vidhiti sauti.

Amesisitiza kuwa katika Takwimu zilizopo Dar es Salaam inawakazi takribani milioni 5.7 amewataka kutengeza miundombinu ya Udhibiti taka.

"Ninazitaka Halimashauri zote ziwe na madampo,Halimashauri zote zitoe Elimu za utenganishaji taka Chupa naUgali "Amebainisha Chalamila. 

Chalamila Ameeleza kuwa Viongozi wa Serikali ya Pugu kinyamwezi kutenga maeneo kuchata taka.

Amebainisha kuwa nivyema Watendaji wa mitaa kudhibiti Mabango,matangazo kwenye Maeneo ambayo hayarusiwi.

Katika Hatua nyingine Mkuu wa Wilaya Kinondoni Sady Mtambule Amewataka   Wananchi kutumia anuani za Makazi  kwa Usahihi. 
Amesema kuwa Anuani za makazi ndio utambulisho wa Wananchi katika ngazi  za juu za Serikali. 

Aidha Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ubungo  Wakili Albert Msando amesema kikao hicho kinalenga kutoa miongozo kwa watendaji wa Serikali za mitaa. 

Amesema kikao hicho nikakao cha kuleta majawabu ya Changamoto zinazowakabili Wananchi. 

" Madiwani wakuu wa Wilaya  watendaji wa Serikali za mitaa ili kuleta majawabu"Amesema Wakili  Msando.   

Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

MWAKIPOSA ASHINDA NAFASI YA UWENYEKITI WA WENYEVITI WA SERIKALI YA MTAA MKOA WA DAR ES SALAAM

DKT. KIJAZI KUSIMAMIA MIRADI YA MAENDELEO JIMBO LA KOROGWE MJINI.