TAASISI ZATAKIWA KUIMARISHA KITEKNOJIA KUFIKIA DIRA 2050.
Timothy Marko DmNews Online
DAR ES SALAAM.KATIKA
KUHAKIKISHA Dira ya Maendeleo ya 2050 inatekelezwa ,Taasisi za Umma Nchini zimetakiwa kuwapa nafasi watumishi wa Umma mafunzo na Ujuzi kwenye vyuo mbalimbali vya Utumishi wa Umma ili kuleta Ufanisi katika kazi zao.
Akimwakilisha Makamu wa Rais wa Jamuhuri Muunganowa Tanzania Dkt.Emanuel Nchimbi katika Kongamano la Watumishi wa umma Nchini Leo,Juni 18,2026 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti Utumishi wa Umma na Utawala Bora Ridhiwan Kikwete amesema kuwa lengo la Kongamano hilo ni Utekelezaji wa Maazimio ya Dira ya Maendeleo ya 2050 yanayolenga kukuza Maarifa Uwajibikaji na
Ufanisi baina ya Watumishi wa umma Nchini.
"Kongamano hili pia linalenga kutathimini Utumishi wa Umma katika kutekeleza Dira ya Maendeleo ya 2050"Amesema Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti Utumishi wa Umma na Utawala Bora Ridhiwan Kikwete.
Waziri wa Utumishi wa Umma Kikwete Ameongeza kuwa kutokana na mabadiliko ya kasi ya Teknolojia, Watumishi hawanabudi kujiendeleza ilikuweza kukuza Ufanisi.
Amesisitiza kuwa nivyema Taasisi zikaboresha eneo la Tafiti katika kuimarisha Miongozo ya Taasisi zao.
"Nivyema Watumishi wa umma wakahudhulia mafunzo ya lazima katika vyuo ilikukuza Ufanisi "Amebainisha Kikwete.
Aidha kwa upande wake Waziri wa Katiba Utumishi Umma wa Zanzibar Haroon Suleiman amesema kuwa Kongamano hilo lenye kauli mbiu Utumishi wa Umma kufanikisha Dira ya Maendeleo ya 2050 nakubainisha kuwa Dira peke yake katika Utekelezaji wa Sera halitoshi bali ikuweza kuikamilisha Dira hiyo inahitaji Watumishi wenye Weledi.
Amesema Nivyema Taasisi zote zitakazo hudhurilia Mkutano huo kuchukua mawazo yatakayo patikana na kufanya Utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya 2050.
"Vyuo vyetu tunaimarisha mafunzo yatakayoleta maarifa kwa Watumishi ,ilikuweza kupata Watumishi wenye Weledi"Waziri wa Katiba na Utumishi wa Umma Zanzibar Amesema Haroon Suleiman.
Naye Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Dkt.Albert Maboresho amesema Kongamano hilo ni mwendelezo jitihada zilizo asisiwa 2025 katika kukuza Ubunifu matumizi ya Teknolojia.
Amesema katika kufanikisha Dira 2050 kuhakikisha Utekelezaji wa kitasisi katika Utekelezaji wa Dira 2050.
"Kongamano hili ni la pili kitaaluma la Utumishi wa Umma nijitihada 2025,katika kukuza Teknolojia na Ubunifu "Amebainisha Haroon Suleiman.

Comments
Post a Comment