Posts

MLIOKUWA WABUNGE KARIBUNI URAIANI.RAIS SAMIA AVUNJA RASMI BUNGE.

Image
Na Mwandishi Wetu,DmNewsonline                      DODOMA RAIS  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Juni 27 ,2025 amelihutubia Bunge la jamhuri ya Muungamo wa Tanzania  wakati akilivunja Bunge  hilo la 12. Akihutubia Bunge ambalo lililokuwa  likiongozwa na mwanamama Dkt.Tulia Akson na kusaidiwa na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la ilala Musa Azan Zungu.rais Dkt.Samia alieleza mambo mbalimbali ambayo yamefanywa katika kipindi chake Cha uongozi huku akimpongeza sipka kwa ueledi wake wa kuliomgoza. Amesema wakati anaichukua nchi miaka minne iliyopita kulikuwa na miradi mbalimbali ambapo wakati akihutubia Bunge kwa mara ya Kwanza alihaidi kutekeleza jambo ambalo amelifanya kwa kiwango kikubwa.  Ikumbukwe kuwa Rais Dkt.samia amelivunja bunge rasmi na tayari kuashiria kwa kipyenga Cha uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 ambapo watanzania watapa nafasi ya kuchagua viongozi wao katika ngazi ya ...

RAIS DKT SAMIA AMPONGEZA DKT. TULIA: ASEMA NI KIONGOZI SHUPAVU. "

Image
HAKIKA HAUJATUANGUSHA WANAWAKE WENZIO Na Mwandishi wetu,DmNewsonline                DODOMA _BUNGENI RAIS Dkt. Samia Suluhu Hassan, amempongeza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson, kwa uongozi bora na usimamizi mahiri wa shughuli za Bunge la Kumi na Mbili, akieleza kuwa amekuwa mfano wa kuigwa kwa wanawake nchini. Akihutubia Bunge leo tarehe 27 Juni 2025, Rais Samia ametoa pongezi hizo kwa Spika Dkt. Tulia kwa mafanikio makubwa katika kuongoza na kufanikisha mikutano yote 19 ya Bunge hilo hadi kukamilika kwake kwa ufanisi mkubwa. “Najua haikuwa kazi rahisi, lakini ni kazi nyepesi kwako. Kwa uhodari mkubwa umeifikisha mashua yetu salama bandarini, kama manahodha makini wanavyofanya. Hakika haujatuangusha sisi wanawake wenzio,” amesema Rais Samia. Aidha, ameongeza kuwa Spika Dkt. Tulia, akiwa mwanamke wa pili kushika nafasi hiyo ya juu katika muhimili wa Bunge, ameonesha ...

‎Emirates returns to The Championships, Wimbledon 2025 ‎

Image
By Correspondent, DmNewsOnline ‎Courts are buzzing with the start of The Championships, Wimbledon, and taking place from 30th June – 13th July at The All England Lawn Tennis Club. ‎ ‎Emirates is returning as Official Airline Partner of the event, once again serving ‘fly better’ experiences both in the air and on the ground. ‎ ‎Kick starting a bumper summer of sport, Emirates will be celebrating The Championships via Wimbledon inspired menus onboard flights between Dubai and the UK, branded beverage coasters and headrests across all different cabins, and even offering tennis fans the chance to win a holiday to Dubai via its on the ground interactive booth at the event. ‎ ‎Emirates’ passengers will be in for a treat at 40,000 feet with specially curated Pimm’s cocktails and strawberry mocktails, and strawberries and cream for dessert served in the A380 Onboard Lounge. ‎ ‎Economy and Premium Economy Class passengers travelling with Emirates between the UK and Dubai from now until...

NCHI ZA SADC ZAKUTANA KUJADILI HALI YA USALAMA

Image
Na Angelina Mganga,DmNewsOnline                 BDAR ES SALAAM  KATIKA kuhakikisha hali ya Usalama katika nchi za  Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ,nchi hizo zimekutana katika kikao na kukubaliana kwa pamoja kwa kushirikiana na kuona namna ya  kukabiliana na  majangiri wa wanyamapori ili wawe salama Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 26,2025 Jijini Dar es Salaam, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Dkt.Maduhu Isaac Kazi,amesema kuwa Moja ya agenda ya mkutano huo ni kujadili masuala ya uhamiaji,huduma za wakimbizi pamoja na wanyamapori ili kukabiliana na majangili kwa kufanya kazi kwa pamoja. "Katika kikao hicho wamesisitiza zaidi jinsi ya utunzaji wa wanyamapori ambapo wamekubaliana namna ya kukabiliana na majangili ambao wanaingia kwenye maeneo ya wanyamapori kwa kufanya kazi kwa pamoja kuhakikisha wanyamapori wetu wanakuwa  salama "amesema Dkt. Maduhu Kazi Pia amesema kwamba katika k...

CCM TABORA WAPONGEZA KUBORESHWA HUDUMA ZA AFYA

Image
Na Allan Kitwe, DmNewsonline                   TABORA  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Tabora kimeridhishwa na maboresho makubwa ya miundombinu ya afya katika zahanati, vituo vya afya na hospitali za wilaya zote za Mkoa huo hali iliyopelekea wananchi kuanza kupata huduma bora. Pongezi hizo zimetolewa jana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora Saidi Juma Nkumba alipokuwa akiongea na mwandishi wa gazeti hili baada ya kuhitimishwa ziara ya Kamati ya Siasa ya Mkoa katika wilaya zote. Amesema kuwa huko nyuma vituo vingi vya kutolea huduma za afya katika Mkoa huo vilikabiliwa na changamoto nyingi sana ikiwemo uchakavu wa miundombinu, ukosefu wa dawa na vifaa tiba vya kutosha na uchache wa watoa huduma. ‘Katika kipindi cha miaka 5 ya serikali ya awamu ya 6 inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan miundombinu ya afya imeboreshwa kwa kiwango kikubwa sana ikiwemo kujengwa hospitali mpya kila wilaya na vituo vya afya’, amesema. Nkumba amebainish...

WAZIRI JAFO AMPA PONGEZI WAKILI MSOMI EDWARD OLE LEKAITA.

Image
Na Mwandishi wetu,DmNewsonline                     DODOMA  WAZIRI wa Viwanda na Biashara hapa nchini Seleman Jafo amempongeza Wakili Msomi na Mbunge wa Jimbo la Kiteto Mkoani Manyara kwa kufanya kazi kubwa sana ya kulielimisha Bunge la Tanzania  kupitia ELIMU yake ya USOMI wa SHERIA Jafo ameyasema hayo jijini Dodoma Bungeni wakati alipokua akizungumza juu ya uwekezaji mkubwa wa kiwanda Cha simenti kinachotarajiwa kuwekezwa Kanda ya katika, ambapo mbunge Lekaita ametaka kujua kama ni lini Waziri Jafo  atawapeleka  wawekezaji hao Kiteto kwakua  wananchi wapo tayari kuwapokea.  Jafo amesema Elimu  yake ya usomi wa Sheria imewasaidia sana kama Bunge la Tanzania, ambapo amewataka watu wa Manyara kutambua hilo kuwa  Wana Mbunge makini kutoka katika wilaya ya Kiteto. Aidha Jafo amesema anamuombea ili wananchi wa Kiteto waweze kumrudisha Bungeni kwani amekua ni msaada mkubwa sana  " Naomba nikupongez...

WANAWAKE TABORA WAHAMASISHWA KUWANIA UBUNGE, UDIWANI

Image
Na Allan Kitwe, DmNewsonline               TABORA  ZIKIWA zimebakia siku 123 sawa na miezi 4 kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani hapa nchini, Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoani Tabora umewataka wanawake wote wenye sifa kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu. Wito huo umetolewa jana na Katibu wa Jumuiya hiyo ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoani hapa Rhoda John Madaha alipokuwa akiongea na mwandishi wa gazeti hili ofisini kwake. Amesema kuwa akinamama wana vipaji vingi na uwezo mkubwa wa kuongoza, hivyo anatamani kuona wanawake wengi zaidi mwaka huu wakijitokeza kuchukua fomu punde tu dirisha la utoaji fomu litakapofunguliwa. Rhoda amebainisha nafasi ambazo wanawake wa Tanzania Bara wanaweza kugombea katika uchaguzi huo kuwa ni ubunge wa jimbo, ubunge wa viti maalumu, udiwani wa kata na udiwani wa viti maalumu. ‘Hii ni fursa muhimu sana, naomba akinamama wote wa Mkoa wa Tabora wenye nia, uwezo na sifa zinazotakiwa waje kuc...