NCHI ZA SADC ZAKUTANA KUJADILI HALI YA USALAMA

Na Angelina Mganga,DmNewsOnline

                BDAR ES SALAAM 

KATIKA kuhakikisha hali ya Usalama katika nchi za  Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ,nchi hizo zimekutana katika kikao na kukubaliana kwa pamoja kwa kushirikiana na kuona namna ya  kukabiliana na  majangiri wa wanyamapori ili wawe salama

Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 26,2025 Jijini Dar es Salaam, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Dkt.Maduhu Isaac Kazi,amesema kuwa Moja ya agenda ya mkutano huo ni kujadili masuala ya uhamiaji,huduma za wakimbizi pamoja na wanyamapori ili kukabiliana na majangili kwa kufanya kazi kwa pamoja.

"Katika kikao hicho wamesisitiza zaidi jinsi ya utunzaji wa wanyamapori ambapo wamekubaliana namna ya kukabiliana na majangili ambao wanaingia kwenye maeneo ya wanyamapori kwa kufanya kazi kwa pamoja kuhakikisha wanyamapori wetu wanakuwa  salama "amesema Dkt. Maduhu Kazi

Pia amesema kwamba katika kikao hicho wamejadili kuhusu uhamiaji kutoka nchi Moja kwenda nchi nyingine katika nchi za Jumuiya ya SADC.

Aidha ,amesema kwa upande wa wahamiaji wameweka utaratibu mzuri kwa watu wanaohama kutoka sehemu moja kwenda nyingine bila kupata shida yoyote hasa hati za kusafiria.

Ameongeza kuwa wakimbizi wanaotoka nchi moja kwenda mchi nyingine wanasaidiwa ili waweze kufika na kuwarudisha kwenye nchi zao wakiwa salama.   


Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE TAMISEMI YAKOSHWA NA UBORA WA MIRADI YA MAENDELEO KIBAHA TC

MAMBO 10 MAZITO YANAYOIANGAMIZA NA KUIZAMISHA CHADEMA 2024/2025