KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE TAMISEMI YAKOSHWA NA UBORA WA MIRADI YA MAENDELEO KIBAHA TC
Na Victor Massngu,DmNewsOnline,
KIBAHA
KAMATI ya kudumu ya Bunge ya Tamisemi imesema kwamba imeridhishwa kwa kiasi kikubwa na miradi ya maendeleo katika sekta ya afya na elimu ambayo imetekelezwa katika Halmashauri ya Kibaha mji kupitia fedha zinazotolewa kutoka serikali kuu na nyingine kupitia makusanyo yanayotokana na fedha za mapato yake ya ndani kwa ajili ya kuwaletea wananchi maendeleo.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa kamati hiyo ya kudumu Justine Kamoga wakati wa kamati hiyo ilipofanya ziara yake ya kikazi siku moja katika Halmaashauri ya mji Kibaha yenye lengo la kugagua na kutembelea miradi mbali mbali ya maendeleo kwa lengo la kuweza kujionea mwenendo mzima wa utekelezaji wake.
Mwenyekiti huyo amesema kwamba wameweza kufanya ziara hiyo kwa ajili ya kuweza kutembelea na kwamba katika sekta ya afya na elimu miradi yote wameona kwamba imejengwa katika ubora na kwamba kitu kikubwa ni kuweka mikakati ya kuendelea kuisimamia miradi hiyo kwa ajili ya maslahi ya wananachi wote ikiwa pamoja na fedha ambazo zinatolewa na serikali.
"Kwa kweli tumeweza kufanya ziara mimi pamoja na kamati yangu ya kudumu katika Mkoa wa Pwani tumepitia miradi mbali mbali na kwamba mingi tumeona ipo katika ubora ambao unaridhisha ikiwemo miradi ya afya na elimu katika Halmashauri ya mji Kibaha ambayo nayo tumejionea na tumeridhika,"amesem Kamoga.
Aidha amesema kwamba pamoja na kutembelea miradi mbali mbali na kuridhishwa aliwataka viongozi na wataalamu kuhakikisha kwamba baadhi ya miradi ambayo bado haijamalizika wajitahidi iweze kukamilika kwa wakati na kwamba miradi amabyo imeonekana kuna baadhi ya kasoro iweze kufanyiwa marekebisho ili wananchi waweze kunufaikia na miradi hiyo ambayo inatekelezwa na fedha za serikali.
Pia amempongeza mkurugenzi wa Halmashauri ya Kibaha mji pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha kwa kuweza kuhakikisha wanasimamia vizuri fedha ambazo zinatolewa na Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan katika suala zima la kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo kwa kuzingatia maslahi na haki za wananchi wa eneo husika.
Aidha katika hatua nyingine ameiagiza Halmashauri ya mji Kibaha kuhakikisha wanaweka misingi imara ya uhakikisha wanazingatia miongozo yote ya fedha amabzo zinazotolewa kutoka serikali katika kutekeleza miradi ya maendeleo kwa maslahi ya wananchi wa eneo husika bila ya kuwa na ubaguzi wowote.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za miko na serikali za mitaa (TAMISEMI) Zainabu Katimba amesema kwamba lengo kubwa la serikali ni kuwahudumia ipasavyo wananchi pamoja na kuona kwamba fedha zinazotolewa na Rasi Dkt Samia Suluhu Hassan zinakwenda kikamilifu katika kutekeleza miradi ya maendeleo.
Aidha Naibu Waziri huyo ambaye aliambatana na kamati hiyo alisema maelekezo yote ambayo amepatiwa na wajumbe wa kamati hiyo kuhusiana na baadhi ya kasoro zilizopo katika miradi ya maendeleo atakwenda kuzifanyia kazi na kuzitafutia ufumbuzi wa kina kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanapata huduma iliyobora kupitia miradi inayotekelezwa katika maeneo yao.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Kibaha mjini Dkt. Rogers Shemwelekwa amesema kwamba anaishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kutenga fedha nyingi ambazo zimeweza kusaidia kwa kiasi kikubwa katika kutekeleza ujenzi wa miradi mipya kabisa katika sekta ya elimu pamoja na afya.
Mganga mkuu wa Halmashauri ya Kibaha mjini Catherine Saguti akisoma taarifa kwa wajumbe wa kamati hiyo ya kudumu ya bunge amebainisha kwamba kutokana na juhudi ambazo zinafanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kitenga fedha zimeweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kujenga mradi mkubwa wa ujenzi wa Hospitali mpya ya Kibaha mji pamoja na vituo mbali mbali vya afya.
Naye Diwani wa kata ya Pangani Agustino Mdachi amemshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa kituo cha afya Pangani ambao utaweza kuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi ambao walikuwa wanapata shida ya kutembea umbari mrefu.
Katika ziara hiyo ya kamati ya kudumu ya bunge ya Tamisemi imeweza kutembelea katika mradi wa hospitali ya Halmashauri ya Kibaha mjini, kujionea ujenzi wa kituo cha afya Pangani, mradi wa shule mpya ya msingi mtakuja,pamoja na kutembelea mradi wa ujenzi wa shule ya mpya ya sekondari Tangini.
Comments
Post a Comment