WAZIRI JAFO AMPA PONGEZI WAKILI MSOMI EDWARD OLE LEKAITA.



Na Mwandishi wetu,DmNewsonline

                    DODOMA 

WAZIRI wa Viwanda na Biashara hapa nchini Seleman Jafo amempongeza Wakili Msomi na Mbunge wa Jimbo la Kiteto Mkoani Manyara kwa kufanya kazi kubwa sana ya kulielimisha Bunge la Tanzania  kupitia ELIMU yake ya USOMI wa SHERIA

Jafo ameyasema hayo jijini Dodoma Bungeni wakati alipokua akizungumza juu ya uwekezaji mkubwa wa kiwanda Cha simenti kinachotarajiwa kuwekezwa Kanda ya katika, ambapo mbunge Lekaita ametaka kujua kama ni lini Waziri Jafo  atawapeleka  wawekezaji hao Kiteto kwakua  wananchi wapo tayari kuwapokea.

 Jafo amesema Elimu  yake ya usomi wa Sheria imewasaidia sana kama Bunge la Tanzania, ambapo amewataka watu wa Manyara kutambua hilo kuwa  Wana Mbunge makini kutoka katika wilaya ya Kiteto.

Aidha Jafo amesema anamuombea ili wananchi wa Kiteto waweze kumrudisha Bungeni kwani amekua ni msaada mkubwa sana

 " Naomba nikupongeze kwanza Wakili Msomi kaka yangu Edward Ole Lekaita, nakuombea sana watu wa Kiteto wakurudishe, Umefanya kazi kubwa sana, Umelielimisha Bunge hili sana , Elimu yako ya Usomi wa Sheria imetusaidia sana kama Bunge la Tanzania, na watu wa Manyara wasikie kwamba tuna Mbunge makini kutoka katika wilaya ya Kiteto, hongera sana ndugu yangu Ole Lekaita" amesema Waziri Jafo.

Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

MWAKIPOSA ASHINDA NAFASI YA UWENYEKITI WA WENYEVITI WA SERIKALI YA MTAA MKOA WA DAR ES SALAAM

KILINDI BARABARA BADO NI CHANGAMOTO