RAIS DKT SAMIA AMPONGEZA DKT. TULIA: ASEMA NI KIONGOZI SHUPAVU. "

HAKIKA HAUJATUANGUSHA WANAWAKE WENZIO

Na Mwandishi wetu,DmNewsonline 

              DODOMA _BUNGENI

RAIS Dkt. Samia Suluhu Hassan, amempongeza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson, kwa uongozi bora na usimamizi mahiri wa shughuli za Bunge la Kumi na Mbili, akieleza kuwa amekuwa mfano wa kuigwa kwa wanawake nchini.

Akihutubia Bunge leo tarehe 27 Juni 2025, Rais Samia ametoa pongezi hizo kwa Spika Dkt. Tulia kwa mafanikio makubwa katika kuongoza na kufanikisha mikutano yote 19 ya Bunge hilo hadi kukamilika kwake kwa ufanisi mkubwa.

“Najua haikuwa kazi rahisi, lakini ni kazi nyepesi kwako. Kwa uhodari mkubwa umeifikisha mashua yetu salama bandarini, kama manahodha makini wanavyofanya. Hakika haujatuangusha sisi wanawake wenzio,” amesema Rais Samia.

Aidha, ameongeza kuwa Spika Dkt. Tulia, akiwa mwanamke wa pili kushika nafasi hiyo ya juu katika muhimili wa Bunge, ameonesha weledi, uthubutu na kujiamini katika utekelezaji wa majukumu yake ya kiuongozi.


Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

MWAKIPOSA ASHINDA NAFASI YA UWENYEKITI WA WENYEVITI WA SERIKALI YA MTAA MKOA WA DAR ES SALAAM

KILINDI BARABARA BADO NI CHANGAMOTO