Posts

VIJANA WA DENMARK WATEMBELEA MRADI WA NYUKI KOROGWE

Image
Vijana sita wa Denmark na wenyeji wao, walipofika Shamba la Nyuki Kwamaraha. Na Yusuph Mussa, DmNewsonline                KOROGWE  VIJANA sita kutoka nchini Denmark wametembelea Mradi wa Nyuki wa Jimbo la Tambarare, Dayosisi ya Kaskazini Mashariki ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) na kujionea maendeleo ya mradi huo wa wanawake na vijana. Pamoja na mambo mengine, vijana hao kutoka vyuo na maeneo mbalimbali nchini Danmark kupitia kikundi chao cha Global Story Tellers, wanatembelea miradi yote Tanzania inayofadhiliwa na Shirika la kidini la Danmission, na kwa Wilaya ya Korogwe, shirika hilo kupitia Shirika la Uhifadhi wa Misitu ya Asili Tanzania (TFCG), imefadhili Mradi wa Nyuki kupitia FORLIVES. Akizungumza kwenye ziara hiyo iliyofanyika Septemba 5, 2026, Mwenyekiti wa Kamati ya Kiuchumi Jimbo la Tambarare, Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Kanisa la KKKT, Betty Munuo alisema Danmission kupitia Mradi wa FORLIVES, baada ya kuwawe...

UJENZI BOMBA LA GESI KISEMVULE-MBAGALA WASHIKA KASI.

Image
Na Mwandishi Wetu, DmNews  DSM TANZANIA imefikia hatua ya kihistoria katika mageuzi yake ya nishati.  Kwa miaka mingi, mazungumzo kuhusu hazina kubwa ya gesi asilia nchini yalijikita zaidi kwenye uwezekano wa baadaye. Leo, uwezekano huo unabadilika kuwa nishati halisi, safi na ya bei nafuu inayotumika barabarani, viwandani na majumbani. Wakati Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) likistahili sifa kubwa kwa kuweka dira ya kimkakati na msingi wa kisera, sifa za utekelezaji zinaelekea kwa kampuni za ndani zinazobadilisha dira hiyo kuwa miundombinu halisi ardhini, ikiongozwa na Rashal Energies Limited. Ujenzi wa bomba la kilomita 22 kutoka Kisemvule hadi Mbagala ulianza rasmi Julai 28, 2026, baada ya vibali na idhini zote za kisheria kukamilika Mei 2026 na maandalizi ya awali kukamilika mwezi Juni mwaka huu. Hadi sasa, kilomita mbili za bomba zimeshaunganishwa, kilomita moja na nusu zimechimbwa mfereji, na sehemu za kwanza tayari zimewekwa ardhini, kufunikwa na kufanyiw...

JAMII YA UFUGAJI MKOANI ARUSHA KUIMARISHA ULINZI KWA WANAWAKE ILI KUONDOKANA NA UKATILI WA KIJINSIA DHIDI YA WANAWAKE.

Image
    Timothy Marko DmNews Online              DAR ES SALAAM.  KATIKA kuhakikisha Ulinzi wa Wanawake Unaimarishwa taasisi ya Pastoral Women's Concil ya Mkoani Arusha (PWC)imesema inaendelea kusambaza Agenda muhimu ya ulinzi wa Wanawake ili kuondokana na Madhira ya ukatili wa kijinsia. Akizungumza Leo,Septemba 8,2026 jijini Dar es Salaam Muwakilishi wa Taasisi ya jumuhia ya Wanawake wafugaji Mkoani Arusha Nalemuta Moisan amesema kuwa katika taasisi yake imekuwa ikitoa mchango wa masuala ya Uongozi kwa Wanawake katika sekta ya kilimo ili kutoa fursa mbalimbali za masula ya sekta hiyo huku suala la ulinzi wa Wanawake dhidi ya ukatili likipewa kipaumbele. "Agenda ya Ulinzi na Amani ni Azimio muhimu katika kujenga fursa kwa Wanawake, Tumekuwa tukishirikiana Serikali katika kutekeleza Agenda hii ikiwemo utatuzi wa Migogoro "Amesema Nalemuta Moisan. Aidha kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Global Peace Foundation (GPF) Hussein Faraji amesem...

VIONGOZI MBALIMBALI WA SERIKALI NA CHAMA WAFIKA KUMPA POLE RAIS DKT. SAMIA KIZIMKAZI MKOA KUSINI UNGUJA VISIWANI ZANZIBAR

Image
    Na Mwandishi wetu, DmNewsonline                ZANZIBAR  MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi, Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba.  pamona na Viongozi wengine mbali mbali wa Vyama na Serikali  Sambamba na Wananchi,  wakimfariji  Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Tanzania mara baada ya kufika  nyumbani kwake Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja, kufuatia kufiwa na Mume wake Maalim Hafidh Ameir Hassan aliyefariki Dunia katika Hospitali ya Mzena Zanzibar,    Sept, 07,2026. 

CCM DAR YAUNGA MKONO MCHAKATO WA KUMPATA MAKAMU WA RAIS, YAMPONGEZA SAMIA.

Image
  Timothy Marko, DmNews online              DAR ES SALAAM  HALIMASHAURI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Mkoa wa Dar es salaam imeunga mkono maamuzi ya Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kuhusu mchakato wa kumpata Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Uamuzi huo umefikiwa baada ya kikao hicho kufanyika Agosti 26,2026, huku CCM Mkoa wa Dar es Salaam ikieleza kuwa maamuzi hayo yamezingatia maslahi mapana ya Taifa pamoja na matakwa ya Katiba ya CCM na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hayo yamebainishwa  leo Septemba 7,2026 na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam  Abbas Mtemvu wakati akizungumza na waandishi wa habari kutoa tamko la maadhimio ya kikao cha Halmashauri kuu CCM Mkoa wa Dar es salaam kilichoketi Septemba 6,2026. Kwa mujibu wa Mtemvu mchakato huo ulizingatia Ibara ya 103(8) ya Katiba ya CCM ya mwaka 1977, kama ilivyorekebishwa,pamoja na Ibara ya 50(2)(c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzan...

WAKULIMA KOROGWE WATOA USHUHUDA WALIVYONUFAIKA NA FORLIVES

Image
  Wakulima wa Kikundi cha Vugiri Farmers Group wakiwa kazini.  Na Yusuph Mussa,DmNewsonline             KOROGWE  BAADHI ya wakulima wa mahindi., maharage, viungo na mbogamboga wa Kijiji cha Vugiri, Kata ya Vugiri, Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga wameelezea mafanikio yao baada ya kuwezeshwa na Mradi wa FORLIVES. Wakulima hao walitoa ushuhuda wao Septemba 4, 2026 mbele ya vijana sita kutoka vyuo na maeneo mbalimbali nchini Denmark kupitia kikundi chao cha Global Story Tellers, wanaotembelea miradi yote Tanzania inayofadhiliwa na Shirika la kidini la Danmission, na kwa Wilaya ya Korogwe, taasisi hiyo kupitia Shirika la Uhifadhi wa Misitu ya Asili Tanzania (TFCG), inafadhili Mradi wa Tunza Uumbaji (Care for Creation). Mkulima wa Vugiri Lishe Group, Judithi Ngomo, alisema Mradi wa FORLIVES  uliwawezesha wananchi kiuchumi kwa kuwapa elimu ya kilimo cha mbogamboga, maharage, mahindi, viungo, ufugaji wa nyuki, kuwapa vifaa kwa ajili ya ulinzi wa ...