JAMII YA UFUGAJI MKOANI ARUSHA KUIMARISHA ULINZI KWA WANAWAKE ILI KUONDOKANA NA UKATILI WA KIJINSIA DHIDI YA WANAWAKE.
Timothy Marko DmNews Online
DAR ES SALAAM.
KATIKA kuhakikisha Ulinzi wa Wanawake Unaimarishwa taasisi ya Pastoral Women's Concil ya Mkoani Arusha (PWC)imesema inaendelea kusambaza Agenda muhimu ya ulinzi wa Wanawake ili kuondokana na Madhira ya ukatili wa kijinsia.
Akizungumza Leo,Septemba 8,2026 jijini Dar es Salaam Muwakilishi wa Taasisi ya jumuhia ya Wanawake wafugaji Mkoani Arusha Nalemuta Moisan amesema kuwa katika taasisi yake imekuwa ikitoa mchango wa masuala ya Uongozi kwa Wanawake katika sekta ya kilimo ili kutoa fursa mbalimbali za masula ya sekta hiyo huku suala la ulinzi wa Wanawake dhidi ya ukatili likipewa kipaumbele.
"Agenda ya Ulinzi na Amani ni Azimio muhimu katika kujenga fursa kwa Wanawake, Tumekuwa tukishirikiana Serikali katika kutekeleza Agenda hii ikiwemo utatuzi wa Migogoro "Amesema Nalemuta Moisan.
Aidha kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Global Peace Foundation (GPF) Hussein Faraji amesema kuwa Agenda ya umoja wa Mataifa 2035 imekuwa ikitolea mkazo Ulinzi wa Wanawake.
Amesema Kutokana na Nchi ya Tanzania kupakana na Nchi nyingi ,kumekuwa na Changamoto Mkoani kigoma ambapo Kuna Changamoto ya ulinzi wa Haki za Wanawake.
"Hatua hii imekuwa ngumu sana katika kupambana na Changamoto za Ukatili dhidi ya Wanawake kutoka kwenye makaratasi kwenda kwenye Utekelezaji "Amesema Mkurugenzi Mkaazi wa Global PEACE foundation Hussein Faraji.

Comments
Post a Comment