CCM DAR YAUNGA MKONO MCHAKATO WA KUMPATA MAKAMU WA RAIS, YAMPONGEZA SAMIA.

  Timothy Marko, DmNews online

             DAR ES SALAAM 

HALIMASHAURI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Mkoa wa Dar es salaam imeunga mkono maamuzi ya Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kuhusu mchakato wa kumpata Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Uamuzi huo umefikiwa baada ya kikao hicho kufanyika Agosti 26,2026, huku CCM Mkoa wa Dar es Salaam ikieleza kuwa maamuzi hayo yamezingatia maslahi mapana ya Taifa pamoja na matakwa ya Katiba ya CCM na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hayo yamebainishwa  leo Septemba 7,2026 na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam  Abbas Mtemvu wakati akizungumza na waandishi wa habari kutoa tamko la maadhimio ya kikao cha Halmashauri kuu CCM Mkoa wa Dar es salaam kilichoketi Septemba 6,2026.

Kwa mujibu wa Mtemvu mchakato huo ulizingatia Ibara ya 103(8) ya Katiba ya CCM ya mwaka 1977, kama ilivyorekebishwa,pamoja na Ibara ya 50(2)(c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Halikadhalika amesema kuwa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam imempongeza Makamu wa Rais aliyeteuliwa, baada ya kutangazwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuthibitishwa na Bunge na kuapishwa kwa mujibu wa Katiba.

"CCM Mkoa wa Dar es Salaam imemtakia Makamu wa Rais huyo kazi njema na mafanikio katika kutekeleza majukumu aliyoaminiwa na Rais na Mwenyekiti wa CCM,Dkt. Samia Suluhu Hassan.amesema Mtemvu.

Katika hatua nyingine,Halmashauri Kuu hiyo imesema inaunga mkono uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan,huku ikimpongeza kwa kazi kubwa anayoifanya katika kukiongoza chama na kuendesha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Amesema kuwa Chama hicho kitaendelea kuunga mkono juhudi za uongozi wa Dk. Samia, huku ikimtakia afya njema na mafanikio katika kuendelea kulitumikia Taifa.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA ASHINDA NAFASI YA UWENYEKITI WA WENYEVITI WA SERIKALI YA MTAA MKOA WA DAR ES SALAAM

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

WAMILIKI WAMASHAMBA SOMELO_ ZINGIZIWA WAJA JUU WASEMA KUNA MTU ANATAKA KUPORA MAENEO YAO ,WATISHIA KWENDA MAHAKAMI.