VIJANA WA DENMARK WATEMBELEA MRADI WA NYUKI KOROGWE

Vijana sita wa Denmark na wenyeji wao, walipofika Shamba la Nyuki Kwamaraha.

Na Yusuph Mussa, DmNewsonline

               KOROGWE 

VIJANA sita kutoka nchini Denmark wametembelea Mradi wa Nyuki wa Jimbo la Tambarare, Dayosisi ya Kaskazini Mashariki ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) na kujionea maendeleo ya mradi huo wa wanawake na vijana.

Pamoja na mambo mengine, vijana hao kutoka vyuo na maeneo mbalimbali nchini Danmark kupitia kikundi chao cha Global Story Tellers, wanatembelea miradi yote Tanzania inayofadhiliwa na Shirika la kidini la Danmission, na kwa Wilaya ya Korogwe, shirika hilo kupitia Shirika la Uhifadhi wa Misitu ya Asili Tanzania (TFCG), imefadhili Mradi wa Nyuki kupitia FORLIVES.

Akizungumza kwenye ziara hiyo iliyofanyika Septemba 5, 2026, Mwenyekiti wa Kamati ya Kiuchumi Jimbo la Tambarare, Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Kanisa la KKKT, Betty Munuo alisema Danmission kupitia Mradi wa FORLIVES, baada ya kuwawezesha kwa mafunzo wanawake na vijana zaidi ya 30 kwenye jimbo hilo, Oktoba, mwaka 2025 walianzisha shamba la ufugaji nyuki Kitongoji cha Kwamaligwa, Kata ya Kwamatuku wilayani Handeni lenye ukubwa wa ekari 86.

Lakini pia FORLIVES iliwapa mizinga 19 ya nyuki, nguo za kujikinga (overall) saba, mabuti, mabonba ya moshi ya kutuliza nyuki sita, na tayari wameanza kuvuna asali kilo 18, lakini Desemba, mwaka 2026 wanatarajia kuvuna zaidi asali sababu karibu mizinga yote ina nyuki.

Munuo alisema FORLIVES chini ya Meneja wa Shirika la TFCG Wilaya ya Korogwe, Bettie Luwuge, pia iliwapatia ndoo 15 za kuhifadhi asali, ambapo ndoo ni sita, na madumu tisa. Pia vifungashio vya asali 300.

"Kutokana na wananchi kuhamasika, waumini wa Usharika wa Korogwe nao wakaweka mizinga ya nyuki 20, na Washirika wa Mtaa wa Bagamoyo nao wakaweka mizinga 10. Kwa ajili ya usalama, kwa sasa mizinga imewekwa kwenye shamba la mzee Mcharo, Kitongoji cha Kwamaraha (Handeni), wakati tukijenga nyumba ya kudumu kwenye shamba letu lililopo Kwamaligwa (Handeni)" amesema Munuo.

Munuo amewashukuru Danmission kwa ufadhili huo, kwani umelenga kuinua kipato cha mwananchi mmoja mmoja, na kuomba kama kutatokea fursa ya ufadhili wa miradi mingine, basi waweze kuwafikiria tena.

Mchungaji John Ndimbo, Mkuu wa Jimbo la Tambarare, Kanisa la KKKT, Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, alitoa shukrani kwa vijana hao kufika Makao Makuu ya Jimbo hilo yaliyopo Korogwe mjini, na pia kwenda kuona shamba la nyuki, na kusema mradi huo umeleta neema kwa wananchi sababu matokeo yameanza kuonekana.
       Mizinga ya nyuki.
Wakiangalia mizinga ya nyuki.

Betty Munuo (kushoto) akitoa maelezo kwa wageni.

 Mchungaji John Ndimbo, Mkuu wa Jimbo la Tambarare, Kanisa la KKKT, Dayosisi ya Kaskazini Mashariki.   

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA ASHINDA NAFASI YA UWENYEKITI WA WENYEVITI WA SERIKALI YA MTAA MKOA WA DAR ES SALAAM

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

WAMILIKI WAMASHAMBA SOMELO_ ZINGIZIWA WAJA JUU WASEMA KUNA MTU ANATAKA KUPORA MAENEO YAO ,WATISHIA KWENDA MAHAKAMI.