WAZIRI MKUU NCHEMBA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA BARAZA LA MAWAZIRI USAFIRI MAJINI AFRIKA (MOESNA)
Timothy Marko ,DmNews Online .
DAR ES SALAAM.
WAZIRI Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Mwigulu Lameck Nchemba anatarajiwa kuwa Mwenyeji wa Mkutano wa (10) wa Kawaida wa Baraza la Mawaziri la Shirika la Masuala Usafiri Majini kwa Nchi za Mashariki,Kusini, na Kaskazini mwa Afrika (MOESNA).
Akizungumza Leo October 13,2026 jijini Dar es Salaam Naibu waziri wa Uchukuzi David Kihenzile amesema kuwa Mkutano huo unatarajiwa kufanyika katika Hotel ya Johari Rotana jijini Dar es Salaam, ambapo Utajuisha Nchi Takribani (20) za Ukanda wa Bara la Afrika .
"Baadhi ya Nchi zitakazo hudhurilia Mkutano huo nipamoja na Namibia, Congo DRC, Misri,Somalia, Seychelles, Eritrea, Sudan Kusini, Sudan Kaskazini, Zimbabwe, Kenya "Amesema Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile.
Naibu waziri Uchukuzi Kihenzile Ameongeza kuwa Baadhi ya mada zitakazo jadiliwa katika mkutano huo nipamoja na itifaki ya kikanda ya Usafirishaji wa majini kati ya Bandari za Nchi Wanachama na Ushirikiano wa Kampuni za meli za kikanda.
Amesisitiza kuwa Agenda nyingine Nyinginenezo zitakazo jadiliwa nipamoja na Uanzishwaji wa Chuo cha kikanda cha masuala ya Bahari.
"Mpango Mkakati waMOESNA wa miaka mitano wa 2026/hadi 2031,Mikataba wa Uanzishwaji wa Moesna Uliopitiwa upya wa Mwaka 2026,Mfumo wa Ugawaji wa Bajeti kwa Nchi wanachama Uliopitiwa Upya,Sambamba na Utawala wa Sekta yaUsafiri wa Majini,Usalama Baharini na Miunganisho ya kikanda "Amebainisha Naibu waziri wa Uchukuzi Kihenzile.
Kwaupande wake Katibu Mkuu wa Baraza la Mawaziri la Shirika la Masuala ya Usafiri wa Majini kwa Afrika Mashariki, kusini na Kaskazini (MOESNA)Kassim Mpaata amesema Mkutano huo umeadhimia kujadili Juu ya ushirikiano wa kikanda katika kuimarisha na kuongeza nafasi ya Afrika katika Uchumi wa kimataifa unaotegemea Shughuli za Usafiri wa majini
"Mkutano huu unatarajiwa kushughulikia changamoto za muda mrefu ikiwemo Gharama za Usafirishaji wa mizigo, Ushiriki mdogo wa kampuni zinazomililkiwa wa Afrika, pamoja Miunganishoya Usafiri Majini "Amesema Mpata.

Comments
Post a Comment