PROF. MAPESA AFUNGUA KONGAMANO LA TANO NA KUZINDUA KITABU CHENYE MKUSANYIKO WA MAKALA ZA KITAALUMA
Na Mwandishi wetu,DmNewsonline DAR ES SALAAM MKUU wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof. haruni Mapesa leo amezindua kitabu kinachohusu kumuenzi hayati baba wa Taifa Mwalimu J.K.Nyerere katika kongamano la Tano la Kitaaluma lililofanyika katika Kampasi ya Kivukoni jijini Dar es Salaam. Akizungumza wakati akizindua kitabu hicho Prof. Haruni Mapesa amewaalika watanzania na wanazuoni kutumia hazina kubwa ya Machapisho ya Vitabu vilivyopo katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ili kupata maarifa ya kifalsafa, Maono na Itikadi mbalimbali ambazo baba wa Taifa aliishi nazo. Prof. Mapesa amesema kuwepo kwa kongamano la kumtafakari baba wa Taifa inatoa fursa kwa wadau mbalimbali kuyajadili na kuyapitia yale yote yaliyofanywa na Muasisi wa Taifa la Tanzania, kwa lengo la kuyaenzi na kuyaendeleza. Mkuu huyo wa Chuo ameitaja Mada kuu ya Kongamano hilo kuwa ni “URITHI WA MWALIMU NYERERE KATIKA UJENZI WA JAMII HIMILIV...