BOT: TANZANIA YABORESHA SERA ZA KIUCHUMI KUKABILIANA NA EL NIÑO

  Timothy Marko, DmNewsonline

           DAR ES SALAAM

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imesema inaendelea kuboresha sera zake za fedha ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi, ikiwemo hali ya hewa ya El Niño, pamoja na changamoto zinazotokana na mgogoro wa Mashariki ya Kati.

Gavana wa BoT, Emanuel Tutuba, amesema mikakati hiyo inalenga kuhakikisha upatikanaji wa fedha na mikopo kwa ajili ya kuendeleza shughuli za kiuchumi na miradi ya maendeleo, huku uchumi ukiendelea kuwa na uwezo wa kukabiliana na misukosuko.

Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam  Oktoba 8,2026, Gavana Tutuba amesema miongoni mwa mikakati ya benki hiyo ni kuongeza akiba ya fedha za kigeni pamoja na ununuzi wa dhahabu kutoka kwa wachimbaji nchini.

Amesema BoT imenunua takribani tani 35.4 za dhahabu katika kipindi cha hivi karibuni, ambapo tani tano tayari zimeuzwa.

“Hadi sasa tumebakiwa na tani 30 za dhahabu ili kuweza kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi, ikiwemo El Niño,” amesema Gavana Tutuba.

Aidha, amesema BoT ina ukwasi wa kuwezesha utoaji wa mikopo kwa kiwango cha asilimia 32.5, huku akisema riba katika baadhi ya benki za biashara imefikia asilimia 6.25.

Kuhusu athari za mgogoro wa Mashariki ya Kati, Gavana Tutuba amesema Serikali imeendelea kuhakikisha upatikanaji wa mafuta, licha ya mabadiliko ya bei katika soko la dunia.
Amesema bei ya pipa moja la mafuta imekuwa katika wastani wa kati ya dola 62 na 108 za Marekani.

“Kiwango hiki ni kizuri kwa ukuaji wa uchumi na kinawezesha shughuli mbalimbali za kiuchumi kufanyika,” amesema.

Gavana Tutuba pia amesema mfumuko wa bei nchini umeendelea kuwa katika kiwango cha asilimia 3.7, licha ya changamoto zinazoendelea katika uchumi wa dunia.

Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

MWAKIPOSA ASHINDA NAFASI YA UWENYEKITI WA WENYEVITI WA SERIKALI YA MTAA MKOA WA DAR ES SALAAM

WAMILIKI WAMASHAMBA SOMELO_ ZINGIZIWA WAJA JUU WASEMA KUNA MTU ANATAKA KUPORA MAENEO YAO ,WATISHIA KWENDA MAHAKAMI.