RAIA WA UTURUKI, KENYA WAKAMATWA WAKISAFIRISHA DAWA ZA KULEVYA
Timothy Marko, DmNewsOnline
DAR ES SALAAM
MAMLAKA ya Kudhibiti na kupambana na Dawa za kulevya Nchini (DCEA) imewakamata raia wa Uturuki,akiwa na grams 1.87 za bangi aina ya skanka Sambamba na Raia wa Kenya wakiwa na grams 3.89za mirungi huku raia wa Nigeria akishikiliwa na Mamlaka hiyo akiwa na gramsb4.6 za bangi .
Operesheni hiyo ilifanyika katika eneo la Ukaguzi wa abiria katika Bandari ya Dar es Salaam ili kubaini matukio ya Usafirishaji wa dawa za kulevya kupitia abiria.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Leo,September 29,2026 Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti na kupambana na Dawa za kulevya Nchini Tanzania (DCEA) Aretas Lyimo amesema kuwa katika operesheni hiyo iliyofanyika mkoani Arusha Mamlaka iliweza kuwakamata raia wawili wa Afrika kusini wakiwa na jumla ya grams 65.8 za Skanka.
"Operesheni hii ilifanyika katika mikoa 14 katika kipindi cha Julai hadi September 2026,katika mikoa ya Dar es Salaam, Kilimanjaro, Arusha, Morogoro, Tabora, Shinyanga, Mwanza, Mara ,Dodoma, Mbeya, Lindi ,Mtwara na Ruvuma "Amesema Kamishina wa Mamlaka ya Kudhibiti na kupambana na Dawa za kulevya Nchini Tanzania (DCEA) Areta Lyimo.
Kamishna Lyimo Ameongeza kuwa katika Operesheni iliyofanywa na Mamlaka hiyo ilibaini pikipiki na mabasi ya abiria iliweza kutumika kusafirisha Dawa Aina ya Mirungi katika mikoa ya Tanga,Kilimanjaro, Arusha, na Dodoma ambapo Dawa aina ya mirungi yenye Uzito wa kilogramu 125.33 huku wa tuhumiwa watatu waliweza kusafirisha Dawa hizo za kulevya kwa kutumia basi ya RATCO lenye namba za Usajili T.443 lilokuwa likifanya safari zake kati ya Tanga na Dar es Salaam.
Amesisitiza Kuwa katika Operesheni hiyo iliiweza kuwakamata Watuhumiwa watatu wakiwa na Bunda za mirungi 238, zenye uzito wa kilogramu 125.33
"Mamlaka inawataka wamiliki na waendeshaji wa mabasi ya Abiria kuimarisha Udhibiti wa mizigo, Ukaguzi wa vyombo vya usafiri pamoja usimamizi wa wafanyakazi ili kuweza kuzuia vyombo vyao kutumia katika kusafirisha Dawa za kulevya "Amebainisha Kamishina 










Comments
Post a Comment