MAPUNG'O FOUNDATION YAIPA NYAKAGWE MSINGI SUKARI KILO 250, MAHINDI GUNIA 15 KWA UJI

  Na Mwandishi wetu,DmNewsonline

                   GEITA

                 
TAASISI  ya Mapung'o Foundation imekabidhi msaada wa sukari kilo 250 na magunia 15 ya mahindi kwa Shule ya Msingi Nyakagwe iliyopo Kata ya Butobela, Jimbo la Busanda, Wilaya ya Geita kwa ajili ya mpango wa uji shuleni

Akizungumza baada ya kukabidhi msaada huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Mapung'o Foundation, Marco Victar, amesema taasisi hiyo imeamua kusaidia baada ya kubaini changamoto ya upatikanaji wa chakula shuleni, lengo likiwa ni kupunguza mzigo kwa wazazi na kuwasaidia wanafunzi kujifunza katika mazingira bora

Naye Afisa Elimu wa Kata ya Butobela aliishukuru Mapung'o Foundation kwa msaada huo na kuwataka wanafunzi kuhudhuria masomo kwa bidii, akisema changamoto ya uji shuleni imepata suluhisho kubwa kupitia mchango huo.

Nao baadhi ya wanafunzi  wameishukuru taasisi hiyo Kwa msaada huo kwani unakwenda kuwa msaada kwao kwenye eneo la Uji wakiwa shuleni hapo.   

Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

MWAKIPOSA ASHINDA NAFASI YA UWENYEKITI WA WENYEVITI WA SERIKALI YA MTAA MKOA WA DAR ES SALAAM

WAMILIKI WAMASHAMBA SOMELO_ ZINGIZIWA WAJA JUU WASEMA KUNA MTU ANATAKA KUPORA MAENEO YAO ,WATISHIA KWENDA MAHAKAMI.