MAKONDA: TUNATARAJIA KUKAMILISHA MAANDALIZI YA AFCON IFIKAPO DESEMBA MWAKA HUU.
Timothy Marko DmNewsOnline
DAR ES SALAAM.
WAZIRI wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo Paul Makonda amesema maandalizi ya AFCON yanatarajiwa kukamilika Desember Mwaka huu.
Akizungumza Leo September 24,2026 na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Paul Makonda amesemakuwa sambamba hilo Serikali imepanga kutumia Shirika la ndege Air Tanzania kuwa chanzo cha Usafirishaji kwa Wachezaji katika Michuano ya AFCON 2027.
"Tunampango wakuweka visa ya pamoja tuna makubaliano na Wizara ya Mambo ndani na Wizara ya Mambo ya Nje " Amesema Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo Paul Makonda.
Makonda Ameongeza kuwa kuelekea Michuano hiyo ya AFCON ujenzi wa Uwanja wa Arusha umefikia Asilimia 95.
Amesisitiza kuwa Tayari Serikali imeshatenga Fedha kwa ajili ya miundombinu ya AFCON.
"Moja ya Mashariti ya Uwanja ya Ubora wa AFCON Uwanja lazima uwe nauwezo kupata Internate ilikuweza kurahisisha Shughuli ndani ya Uwanja kufanyika kwa ufanisi "Amebainisha Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo Makonda.

Comments
Post a Comment