LUSHOTO WAMSHUKURU RAIS SAMIA MRADI WA SOKO NA STENDI
WAZIRI wa TAMISEMI, Profesa Riziki Shemdoe akizungumza na wananchi wa Lushoto. Na Yusuph Mussa, DmNewsonline Lushoto WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Profesa Riziki Shemdoe, amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kutoa sh. bilioni 6.4 kwa ajili ya ukarabati wa Soko Kuu na Stendi Kuu ya Mabasi Lushoto mjini. Ameyasema hayo Julai 22, 2026 kwenye hafla fupi ya utiaji sahihi wa mikataba ya miradi ya uboreshaji wa ujenzi wa Soko Kuu la mjini Lushoto na ujenzi wa Stendi Kuu ya Mabasi, na Msimamizi Mshauri wa Miradi ya ujenzi na uboreshaji wa soko pamoja na ujenzi wa stendi ya mabasi iliyofanyika pembezoni mwa soko hilo. "Tunamshukuru sana Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia sisi wana Lushoto tuweze kupata sh. bilioni 6.4 kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa miundombinu mipya ya Soko la Lushoto pamoja na ujenzi wa stendi mpya ya Lushoto. Niushukuru sana uongozi wa M...