ASILIMIA 80 KUFIKIWA NA NISHATI SAFI IFIKAPO 2034
Timothy Marko Dm Newsonline
DAR ES SALAAM.
KATIKA kuhakikisha Malengo ya kuhakikisha Asilimia 80 ya Watanzania wanakuza matumizi ya Nishati safi yakupikia ifikapo 2034 Serikali imezitaka Asasi za kirahia pamoja na Vyombo vya Habari kukuza Uelewa wa Umuhimu wa Nishati hiyo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Julai 14,2026jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Chama Cha Wafanyabishara wa mitungi ya kuhifadhi Gesi ya LPG Nchini (Tanzania LPG Association) Amos Jackson amesema hadi sasa watanzania milioni 14.8 ndio wanaotumia Nishati hiyo huku adhima ya Serikali kufikia 2034 zaidi ya Asilimia 80 wawe watumiaji wa Nishati hiyo.
"Hadi Sasa Nchi ya China ndio inayoongoza kwa matumizi ya Nishati safi yakupikia ikiwa na watu takriban Bilioni 1.5 wanaotumia Nishati Safi,ikifuatiwa na Nchi ya India "Amesema Mkurugenzi wa TZLPGA) Jackson.
Mkurugenzi Jackson Ameongeza kuwa katika Bara la Afrika Nchi zinazoongoza kwa matumizi ya Nishati safi ya kupikia nipamoja na Misri,Morocco, Nigeria na Tanzania.
Amesisitiza kuwa idadi ya watanzania ambao hawatumii Nishati hiyo nitakribani milioni 16.
Naye Mratibu wa Kitaifa wa kuhamasisha Matumizi ya Nishati safi Nchini (Women In LPG ) Winner Lukumay amesema tathimini inaonesha kuwa kumekuwa na Upungufu wa Watumiaji wa Nishati hiyo ni kutokana na kuwepo kwa Gharama kubwa za kununua mitungi ya gesi pamoja na miundombinu yake hali inayopelekea Baadhi ya Wananchi kutomudu Nishati hiyo.
Amesema kuwa Sambamba na hilo "kumekuwa na uzaji wa Gesi usiokidhi Viwango vya mtumiaji wa Nishati hiyo.
na Kumekuwa na Ufungwaji wa vifaa vya Gesi ikiwemo mitungi isiyokidhi Ubora na Viwango vya Kimataifa. "Amebainisha Lukumay.
Naye Balozi wa Nishati safi ya kupikia ambaye ni Mwigizaji wa Filamu za kibongo Abdullah Mkumbila (Muhogo Mchungu) amesema kuwa Wasani Nchini wana mchango mkubwa katika kuhamasisha jamii kutumia Nishati safi
Amesema Baadhi ya Wananchi wengi wao wanatumia nishati Chafu hali inayowaathiri hasa wakina mama.
"Wakina mama wengi wamekuwa na Macho Mekundu kutokana na Baadhi yao wanatumia Nishati Chafu" Amesema Muhogo mchungu 





Comments
Post a Comment